Thursday, January 29, 2015

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU 15 KISIWANI UNGUJA NA PEMBA LEO.


 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Vuai Ali Vuai kuelekea kukishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.

Kinana amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12. 

Katika ziara hiyo,Ndugu Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara, hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona. 

Katika ziara hiyo ,Ndugu Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Ndugu Kinana kwa ziara yake, kwamba imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama visiwani.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki upandaji wa Mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM-Kusini Pemba,Bakari Mshindo akielekea kushiriki upandaji wa Migomba katika shamba la Ushirika  la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji Migomba katika shamba la Ushirika  la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na mmoja wa viongozi wa Ushirika huo alieleza mbele ya Kinana kuwa Ushirika huo una jumla ya watu 25,na wanajishughulisha na ufugaji wa Kuku wa Kienyeji,Mboga mboga pamoja na Migomba katika shamba lenye ekari mbili na nusu.

Komredi Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa chama na serikali wakiomba dua walipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Hayati Dk. Omari Ali Juma eneo la Wawi Digilini, Wilaya ya Chakechake, Pemba.

Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
Komredi Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa chama na serikali wakiomba dua walipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Hayati Dk. Omari Ali Juma eneo la Wawi Digilini, Wilaya ya Chakechake, Pemba.

Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya mara baada ya kusomewa na kukabidhiwa taarifa fupi ya uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Wilaya na Mkoani.
 Pichani ni moja ya Jengo la tawi ya ofisi ya CCM Milimuni ambapo katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alishiriki ujenzi wake,katika jimbo la Chambani,wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.
 Balozi wa shina namba moja ,Balozi Ame Vuai Shein akisoma taarifa yake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kumtembelea katika kijiji cha Kadarani Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,kusini Pemba.
 Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),alipokuwa akihutubia jioni leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba  jioni ya leo, ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment