Sunday, January 4, 2015

DKT. SHEIN AFANYA UFUNGUZI WA BARABARA UMBUJI,ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji Viongozi wakati alipowasili leo katika uzinduzi wa Barabara ya Njia nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua Barabara ya Njia Nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja leo iliyojengwa na Serikali kupitia kitengo cha Idara ya ujenzi Barabara UUB ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kulia) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji na (kushoto) Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya kufungua Barabara ya Njia Nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja leo iliyojengwa na Serikali Mapinduzi kupitia kitengo cha Idara ya ujenzi Barabara UUB ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Viongozi mbali mbali wakitembea katika Barabara ya Njia NNe -Umbuji Wilaya ya Kati Unguja mara baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Juma Malik Akili,akitoa ripoti ya kitaalamu leo wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Barabara ya Njia Nne -Umbuji Wilaya ya Kati Unguja baada ya kufunguliwa na Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Njia Nne -Umbuji Wilaya ya Kati Unguja baada ya kufunguliwa na Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Barabara ya Njia Nne -Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja zilizofanyika leo kijiji cha Umbuji ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Msoma Risala Farida Rajab akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Njia Nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment