Friday, January 30, 2015

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SimBanking NA FAHARI HUDUMA WAKALA

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’  kupitia kwa mawakala  wa ‘FahariHuduma’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

“Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.

Akielezea namna ya kushiriki  na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

“Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara,” alisema.

Kwa upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa benki hiyo.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wadau wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Maofisa wa Benki ya CRDB.
Wageni waalikwa pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
Maofisi wa Benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja.
Maofisa wa benki ya CRDB.
Ofisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Tawi la CRDB, Kijitonyama, Lucas Busigazi (katikati) kuhusu huduma za benki ya CRDB (kulia) Kulia ni Meneja wa Tawi la Msasani, Saida Francis.
Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza.
Dk. Charles Kimei akisalimiana na wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari (kushoto) akiwa na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakitoka katika Mobile Bank mara baada ya kuzindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia) akiwa na Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu wakiwa katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na wa tatu kushoto ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akijaribu gari aina ya Passo baada ya kuzindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo.

No comments:

Post a Comment