Tuesday, December 2, 2014

Wanafunzi Tisa (9) -Wahitimu mafunzo ya uuguzi na ukunga

Rasilimali watu ni changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya nchini Tanzania. Upungufu huu unaathiri mfumo wa utoaji huduma bora na kwa wakati kwa wahitaji. Upungufu wa wahudumu wa afya  wenye ujuzi unaathiri ngazi zote za huduma na hasa vijijini. Kutokana  na wauguzi wakunga kuwa kiini katika utoaji  huduma za afya   vijijini na mijini kwa ujumla,  kuna umuhimu wa  wakunga hawa kupata elimu ya ujuzi  wa kutosha ili waweze kuwafikia wahitaji zaidi ya asilimia  sabini (70%)  ya  jumla ya wananchi wanaoishi vijijini.

Katika kupambana na changamoto ya upungufu wa wahudumu wa afya hasa katika kulenga  kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, Amref Health Africa imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha taasisi, mashirika na watu binafsi kuchangia mafunzo ya wakunga watalaam   ili waweze kutoa huduma salama, sahihi na kwa wakati ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika wakati wa kujifungua.

Jumla ya Wanafunzi 121 wamehitimu mafunzo ya uuguzi ukunga ngazi ya cheti katika chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga.  Miongoni mwa wanafunzi hao 9 walikuwa wakisoma kwa udhamini wa Barclays bank kupitia kampeni ya “Stand up for African Mothers” inayoendeshwa na Shirika la afya la Amref Health Africa Tanzania.

Barclays Bank ni mshiriki mkubwa katika kampeni hii  na anatoa udhamini wa kusomesha wanafunzi  katika ngazi ya cheti na hivi leo  tumeshuhudia  wanafunzi 9 wamehitimu tayari kwa kwenda kutoa huduma katika jamii zinazowazunguka. Wahitimu hawa wanakwenda kufanya kazi maeneo ya vijijini Kama moja ya lengo na nia ya kampeni ya stand up for African mothers ambayo inalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa maeneo ya kijijini na yaliyo magumu kufikika.

Juhudi za Amref Health Africa na Barclays bank  ni endelevu  na wito unatolewa  kwa mashirika, makampuni ya umma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi  kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga  kwa miaka miwili  yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia

Bank  account at Bank M, Kisutu Branch , Akaunti Namba  0250027331
Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
Mpesa Namba 0762 22 33 48
Tigo pesa Namba 0716 032 441
Airtel money Namba 0685 506306.

Stand Up For African mothers ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuelimisha na kutoa taarifa juu ya umuhimu na mchango wa wakunga wenye ujuzi katika kupunguza viofo vya mama na watoto wakati wa kujifungua.  Kampeni hii inayoendeshwa na Amref Health Africa inalenga kusomesha wakunga 15,000 katika nchi kumi na tatu za Africa wakati Tanzania ikitarajia kusomesha wakunga 3800.
Dr. Pius Chaya,mkuu wa kitengo cha kujenga uwezo Amref Health Africa Tanzania akimuwakilisha Mkurugenzi , Dr. Festus Ilako wakati wa mahafali Chuo hapo.
Jumla ya wanafunzi 121 waliohitimu uuguzi ngazi ya Cheti, miongoni mwao wakiwemo tisa (9) waliofadhiliwa na Barclays kupitia Stand u For African Mothers Campaign inayoendeshwa na Amref Healt.
Mkuu wa Chuo akiwa pamoja na viongozi, wakufunzi wengine katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Chuo, Baba Askofu pamoja na viongozi wa madhehebu mengine katika picha ya pmaoja.

No comments:

Post a Comment