Friday, December 26, 2014

Vodacom Tanzania ilivyowarusha wateja wake kila kona ya jiji la Dar

Mfalme wa muziki wa taarabu na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern taarabu Mzee Yusuf akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki huo katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Gwiji wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wa muziki wake katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Diamond Platnumz mwanamuziki wa kizazi kipya akiwaimbia kwa hisia kali moja ya muziki wake mashabiki wa muziki wake katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Mfalme wa muziki wa taarabu na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern taarabu Mzee Yusuf akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki huo katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Mfalme wa muziki wa taarabu na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern taarabu Mzee Yusuf akicheza na madansa wake wakati wa Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Linex akiimba kwa hisia kali moja ya nyimbo zake kwa mashabiki wake waliofika kwenye”Tamasha la Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika ufukwe wa bahari Coco-beach hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Linex akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika kwenye”Tamasha la Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika ufukwe wa bahari Coco-beach hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva mwenye uwezo mkubwa wa kuimba kwa hisia kali, Sunday Mangu ‘Linex’, juzi Alhamisi alifanya bongo la shoo katika Ufukwe wa Coco (Coco Beach), wakati wa tamasha lililopewa jina la “Vodacom Maisha Murua” ikiwa ni sehemu ya kusheherekea Sikukuu ya Krismasi.

Katika onyesho hilo, Linex aliwapagawisha vilivyo wapenzi wa burudani waliofika kwenye ufukwe huo, ambapo walijikuta wakiimba naye pamoja na kucheza nyimbo zake.

Takribani nyimbo zake zote alizoimba, zilipokewa vizuri na wapenzi hao wa burudani, japo zile za Wema kwa Ubaya, Aifola, Boda Boda, Lekatutigite, Mahakama ya Mapenzi, Mama Halima na nyinginezo.

Mkali huyo wa muziki, alitumia takribani saa moja kufanya shoo yake bila kupumzika, huku akiimba kwa hisia kali kiasi cha wakati fulani kujikuta akitokwa na machozi, hasa pale alipoimba nyimbo za kulalamika kuonewa kama Aifola na Wema kwa Ubaya.

Kitendo hicho kilionekana kuwagusa vilivyo umati uliofurika ufukweni hapo, kiasi cha baadhi yao wakiishia kuinama chini kuonyesha jinsi walivyoguswa na ujumbe uliomo katika nyimbo zake.

Wakati Linex na wasanii wengine chipukizi wakipagawisha katika ufukwe huo, Vodacom ilikuwa ikiwarusha wakazi wa Dar es Salaam katika shoo nyingine iliyopewa jina la Tamasha la Wafalme lililofanyika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala.  

Shoo hiyo iliwahusisha wafalme wawili katika fani ya muziki ambao ni Mfalme wa muziki wa Taarab Mzee Yusuph na mkali wa Bongo Felva, Nasseb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Katika shoo hiyo, wawili hao walifanya mambo makubwa na kukonga vilivyo nyoyo za wapenzi wa muziki waliojitokeza, ikiwamo Diamond kushinda shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor, akiwapiku wenzake kadhaa, akiwamo msanii Ally Kiba na mtangazaji Milady Ayo.

Juu ya matamasha hayo, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, alisema“Vodacom huwa haiwaachi nyuma Watanzania katika kipindi kama hiki cha Sikukuu, huwa tunakuwa nao kuwapa burudani kutimiza kauli mbiu yetu ya ‘Ukiwa na Vodacom Maisha Murua’.”

No comments:

Post a Comment