Thursday, December 4, 2014

TASWIRA: MICHEZO YA BANDARI “INTER-PORTS GAMES” KUFIKIA KILELE KESHO IJUMAA, DISEMBA 05 MJINI MTWARA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Ponsiano Nyami akizungumza na wanamichezo wa Bandari.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bw. Peter Gawile akizungumza na wanamichezo wa Bandari.
Timu kutoka Bandari za Maziwa ikiingia uwanjani.
Timu ya Makao Makuu.
Kikosi cha Bandari ya Dar es Salaam wakijipanga kwa ufunguzi.
Mashabiki wakiwa uwanjani.
Kikosi kazi cha Bandari ya Mtwara kabla ya kuwavaa Bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Ponsiano Nyami akiikagua timu ya Bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwavaa Bandari Mtwara.
Timu ya kuvuta kamba kutoka Bandari ya Dar es Salaam wakimenyana na wenzao wa Bandari Mtwara.
Timu ya kuvuta kamba kutoka Bandari Mtwara wakimenyana na wenzao wa Bandari ya Dar es Salaam.
Maafisa wa huduma ya kwanza kazini.
Timu ya netball kutoka Bandari ya Mtwara.
Timu ya netball kutoka Makao Makuu.
Mchezo wa bao baina ya Makao Makuu na Bandari ya Mtwara.
Mashabiki wakiwa uwanjani Nangwanda Sijaona wakifatilia mechi ya soka kati ya Mtwara na Maziwa.
Matalena Muhagama mkimbiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam akiwa mbele ya wakimbiaji wengine wakati wa michezo ya Bandari ‘Inter-Ports Games’ inayoendelea mjini Mtwara.
Suleiman Mwalilo a.k.a Kingsley kutoka Bandari ya Dar es Salaam akikata upepo katika michezo ya Bandari ‘Inter-Ports Games’
Damian Mkobokwa wa timu ya Makao Makuu na wenzake wakianza mchezo wa kupokezana vijiti.
Mrusha mkuki Ally Mnubi kutoka Bandari ya Dar es Salaam akijiandaa kurusha mkuki.
Mrusha mkuki, Mathias Shija kutoka Bandari za Maziwa akijaribu kete yake katika mchezo huo.
Mrusha mkuki kutoka Bandari Dar es Salaam akijaribu kete yake katika mchezo huo.
Mrusha mkuki Dkt. Hawa Senkoro kutoka timu ya Bandari ya Dar es Salaam.













No comments:

Post a Comment