Wednesday, December 24, 2014

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA IRINGA GNSM ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

MKurungenzi  wa kampuni ya ujenzi  wa barabara Iringa ya GNSM Bw  Geofrey Mungai na mkewe  Sarafina Mungia katikati  wakikabidhi  baada ya misaada  yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 kwa  mlezi  wa  kituo cha yatima Tosamaganga Godfrida Mhongole
Bw Mungai  akishuhudia  jinsi  watoto  wanavyohudumiwa
Bi Sarafina  Mungia na Geofrey Mungai  wakiwatazama wahudumu  wakiwalisha watoto yatima wa Tosamaganga  Iringa
Bw Geofrey Mungai  akisaidia  kuwapa uji  watoto yatima  wa Tosamaganga Iringa baada ya  kumaliza  kuwapa msaada wa chakula  cha Krismas na mwaka mpya
Watoto   wakifurahia msaada  wa chakula
Mlezi  wa  kituo  cha yatima   Tosamaganga  Godfrida Mhongole  kushoto akiwapongeza Mungai na mkewe kwa  msaada wa chakula
Bi sarafina Mungai  akiwa na watoto yatima
majengo ya  kituo hicho
Mtoto akiishangaa  simu ya Bi sarafina
Mungai na mkewe  wakiwa na  watoto  yatima
Mhudumu  wa kituo hicho akimlisha mtoto yatima

Mungai akisaidia  kumnywesha  uji mtoto
Watoto  wakipewa chakula
Mungai na mkewe  wakiwa na watoto  yatima  huku  gari  lililopeleka msaada wa  chakula  likiendelea kushusha
watoto  wakifurahia  msaada  huo


Na matukiodaimaBlog

 MKURUGENZI wa kampuni ya  ujenzi  wa barabara nchini ya  GNSM Contractors Co. Ltd ya mkoani Iringa ametoa msaada  wa chakula chenye  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa  kituo cha kulea watoto yatima  cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa kwa ajili ya  sikukuu ya Krismas na mwaka mpya .


Huku  akiwapongeza   wahudumu  wa  kituo  hicho kwa  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo ya  kulea   watoto  zaidi ya 70 waliopo kituoni hapo kwa moyo wa  kujitoa   zaidi.

Mkurugenzi   huyo Geofrey  Mungai  ambae  aliongozana na mkewe  Bi Sarafina Mungai  alikabidhi msaada   huo jana  ikiwa ni  sehemu ya mwensdelezo  wa kampuni  hiyo na familia yake kuzungukia vituo  mbali mbali  vya yatima kwa  kuwasaidia watoto hao.

Akizungumza  baada ya  kukabidhi msaada  huo  Bw  Mungai  alisema  kuwa  imekuwa ni kawaida  ya kampuni yake kuwakumbuka  watoto  hao  yatima  wa  kituo hicho  na vituo  ikiwa ni moja ya  kuwakumbuka watoto hao  ambao  wanaishi kwa  kutegemea misaada  ya  wasamaria  wema.


Alisema  kuwa jamii inapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto  yatima ambao wanaishi  kwa misaada ya wahisani  wa ndani na nje  baada  kupoteza  wazazi  wao .

Kwani  alisema  kuendelea kuwasaidia  watoto  hao ni kuwasogezea  faraja ya  pekee  ambayo watoto  hao wanahitaji    kutoka kwa  jamii inayowazunguka badala ya kuwasusa  ama  kuwaachia watu  wachache kulea  yatima  hao.

Aidha  alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya makandarasi mkoa  wa Iringa anaendelea  kufanya mazungumzo  na wenzake  ili  kuweka  mpango wa  kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya kuwasaidia misaada  mbali mbali.

Huku  akiishauri  serikali kuangalia  uwezekano kupitia  ofisi  za maendeleo ya   Jamii, Jinsia na Watoto kuweka  utaratibu  wa  kuwakumbuka watoto  waliopo katika  vituo vya yatima kwa  kuwapa mahitaji yao ya  kila  siku .

Bw Mungai  alipongeza  jitihada  kubwa  zinazoendelea  kufanywa na uongozi wa  kituo hicho  cha Tosamaganga ambacho sehemu kubwa watoto  wanaolelewa hapo ni  wale wanaotupwa ama wazazi wao  kufariki baada ya kuwazaa.
 
Alisema  kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea   kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali  wakiwemo makandarasi  wenzake  kuwekeza kwa  watoto hao

Kwa  upande  wake  Bi Sarafina Mungai akizungumza na wahudumu hao  alisema  kuwa kazi wanayoifanya ni kazi  kubwa ambayo serikali na wananchi hawanabudi  kuitambua na  kuwaunga mkono zaidi.

No comments:

Post a Comment