Wednesday, December 24, 2014

MH. ZAINABU KAWAWA AMUENZI HAYATI MZEE KAWAWA KWA VITENDO

Na Mdau Sixmund J.B
Mh Zainabu Kawawa ameamua kuendelea kumuenzi kwa vitendo aliekuwa mmoja wa wahasisi wa Taifa letu Marehemu Baba yake Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwa kuikarabati shule ya msingi aliyo soma Mzee Kawawa. 

Akiwa wilayani Liwale alipokulia na kusomea Marehemu Mzee Kawawa, Mh Zainabu aliwatembela wazee mbali mbali waliokuwa marafiki wa Mzee Kwawa ili kuwawajulia hali na kusikia mitazamo yao ya Liwale ya sasa nakipindi walipo kuwa na Marehemu Mzee Kawawa. 

Wakitoa mitazamo yao Mzee Saidi Mussa Suramoyo na Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi walisema kuwa Mzee Kawawa aliwajali sana watu Waliwale kwani alihakikisha kila mkazi wa wilaya hiyo analima ili apatemazao yakutosha na si kuishi kwa kutegemea wengine, pia alisema Mzee Kawawa aliweza kufanya wanaliwale kuwa kitu kimoja na hakuwagawa tofauti na ilivyo sasa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwagawa wananchi kitu kinacho sababisha mifarakani.

“Sikuizi wanaliwale tunaishi kama hatujuani, watu wanaishi kimakundi makundi tu, tena wale waliokuwa karibu na wakubwa ndio wanafaidi nakuonekana wamaana sana kuliko sisi wazee ambao inaonekana hatuna msaada kwa hao wakubwa, namkumbuka sana rafiki yangu Rashidi Kawawa alitupenda sanaa lakini sasa weacha tu.” Alisema Mzee Saidi Mussa Suramoyo.

Nae Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi akiongea kwa tabu kutokana na uzee aliokuwanao alimshukuru sana Mh Zainabu kwa kufuata nyayo za Baba yake kwa kuwaonesha upendo wa kuwatembelea na hata kuikarabati shule ya Msingi aliyo soma Muhasisi wa Taifa letu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwani ilikuwa katika hali mbaya kimajengo.

Akiongea na Muandishi wa habari hizi, Mh Zainabu aliwashukuru wanaliwale kwa kuishi vyema na Baba yake Mzee Kawawa na kuendelea kumkumbuka kwa mema yote aliyo wafanyia, pia anatoa wito kwa watanzania wote kumuenzi Mzee Kawawa kwa undeleza yale yote mazuri aliyo tuachia hasa la viongozi kuwajali wananchi wanao watumikia.

Mh Zainabu aliwaahidi wazee hao wa Liwale kuendelea kushirikiana nao ili kuyaendeleza yale yote aliyo yafanya mzee Kawawa enzi za uhai wake akiwa kama Mbunge wa wilaya hiyo.
Pichani ni rafiki yake kipenzi cha Hayati Mzee Rashidi Kawawa Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi wa kijiji cha Mpengele akifafanua jambo alipo tembelewa na Mh Zainabu Kawawa ambae ni mototo wa Mzee Kawawa.
Pichani Mwenye furahaa ni Mh Zainabu Kawawa akiwa mbele ya madarasa aliyosomea Baba yake Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwa sasa shule hii inaitwa Shule ya Msingi Kawawa.
Pichani Mh Zainabu Kawawa akiwasikiliza kwa umakini wazee wa kijiji cha Mpengele alipoenda kuwajulia hali.
Mzee Saidi M. Suramoyo akielezea namna walivyo ishi na rafiki yake Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Nyumba hii ndiyo nyumba ya kwanza ya Muhasisi wa Taifa hili Mzee Rashidi Mfaume Kawawa iliyopo kijiji cha Mpirani Wilaya ya Liwale hata hivyo Mzee Kawawa alimzawadia nyumba hii rafikiyake huyu.

No comments:

Post a Comment