Thursday, December 18, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI UMOJA WA VIKUNDI VYA WAMA KATIKA WILAYA YA KINONDONI

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia baadhi ya kazi zinazofanywa na wanavikundi wa UWAMAKI mara baada ya kuwasili kwenye sherehe ya uzinduzi wa vikundi hivyo
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe 
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akisoma maandishi baada ya kuzindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe 
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo huko Chuo Cha Usafirishaji.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo huko Chuo Cha Usafirishaji.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo huko Chuo Cha Usafirishaji.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake mara baada ya kuzindua rasmi Umoja wa vikundi vya WAMA katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe zilizofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji kilichoko eneo la Mabibo
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake mara baada ya kuzindua rasmi Umoja wa vikundi vya WAMA katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe zilizofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji kilichoko eneo la Mabibo
 Baadhi ya wanachama wa umoja wa vikundi vya  WAMA katika wilaya ya Kinondoni wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa umoja wao
 Baadhi ya wanachama wa umoja wa vikundi vya  WAMA katika wilaya ya Kinondoni wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa umoja wao
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa zawadi ya mkeka kutoka kwa wanachama wa vikundi vya WAMA katika wilaya ya Kinondoni, UWAMAKI, WAKATI WA SHEREHE ZA UZINDUZI WA Umoja wao
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti wa Umoja wa vikundi vinavyosimamiwa na WAMA katika wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI), Ndugu Christina Emmanuel wakati alipowasili kwenye Chuo cha Usafirishaji kilichoko eneo la Ubungo kwa ajili ya ufunguzi wa umoja huo. Picha na John Lukuwi

Na Anna Nkinda – Maelezo
Vijana wametakiwa kujiunga na vikundi vya kuweka akiba na kukopa  ili kuchangia mawazo yao  na ubunifu na wakati huo huo wanajitengenezea mazingira ya kujiajiri kwani wengi wao wana elimu na ujuzi walioupata  masomoni lakini wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.

Rai hiyo imetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua Umoja wa Vikundi vya kuweka Akiba vilivyopo chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI) katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Usafirishaji jijini Dar es Salaam. 

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA alisema kupitia vikundi hivyo vijana wanaweza kupata mitaji midogomidogo pamoja na mafunzo ya kuwawezesha kuanzisha biashara na kujiajiri. Kwani mfumo huo wa vikundi na mafunzo ni moja ya njia za kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na hivyo kupunguza tatizo la ajira.

Kwa upande wa wanachama wa UWAMAKI aliwasisitiza  kutoridhika na mafanikio waliyoyapata bali waendelee kutafuta njia za kupiga hatua hususani kupata utaalamu wa kuboresha bidhaa zao , kutafuta masoko zaidi na kufanya ubunifu wa kuweza kuvumbua bidhaa na biashara nyingine tofauti ili kuepukana na ushindani wa soko.

“Mnapokuwa na bidhaa zinazofanana mtakuwa katika mazingira ya kushindania soko jambo ambalo litapunguza kiasi cha mauzo ambayo ndiyo pato lenu wajasiriamali. Jitihada ifanywe ili kuweza kutafuta watalaam ambao watawapa mafunzo ya kukuza biashara”, alisema Mama Kikwete. 

Akisoma risala ya vikundi hivyo Katibu wa UWAMAKI , Mwajuma Waziri aliishukuru Taasisi ya WAMA kwa kuwawezesha  kuwa na vikundi na kupata mafunzo ya kuweka akiba, elimu ya kibenki, usindikaji wa vyakula na huduma ya bima ya afya. 

Waziri alisema, “Kutokana na mafunzo hayo tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali kama vile kutengeneza sabuni za maji za kufulia, sabuni za kuoshea vyombo na kusafishia tairizi, siagi ya karanga na batiki na hatimaye tumeweza kufungua akaunti yetu ya Umoja katika benki ya wanawake (TWB)”.

Katibu huyo alisema walianza na kikundi kimoja kwa kujiwekea hisa moja kwa thamani ya shilingi 1000 pia waliweza kukopesha kiasi cha shilingi 6,300,000 mpaka mwisho wa mwaka walivuna shilingi 12,750,000. 

“Hadi sasa tunavikundi 11 vyenye wanachama 274 kati ya hao wanaume ni wanane katika vikundi hivi  tumeweza kukopesha kiasi cha shilingi 47,500,000/= na kufikia mavuno ya shilingi 79,739,000 kwa mwaka”, alisema.

Alimalizia kwa kusema lengo la kuunda umoja huo ni kushirikiana katika matatizo ya kijamii, kuunda SACCOS na kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Taasisi ya WAMA inasimamia mradi wa kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mafunzo kupitia vikundi katika mikoa ya Dar es Salaam Lindi na  Pwani hadi kufikia Septemba mwaka huu jumla ya watu 18,000 wamefikiwa kwa kupitia vikundi 688 vilivyoundwa na tayari shilingi milioni 227 zimekusanywa na kukopeshwa.



No comments:

Post a Comment