Monday, December 8, 2014

Kilele cha Mbio za Uhuru chafanyika jijini Dar

Mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 katika mashindano ya Uhuru Marathon 2014,Fabian Joseph akimaliza mbio hizo katika viwanja vya Leaders Club,kuliko fanyika kilele cha mbio hizo.Fabian ameibuka kidedea baada ya kuwaacha nyuma washiriki wenzake 10.
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakiingia katika viwanya vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam kumalizia ngwe.
 Washiriki wa mbio fupi za kilometa 21 (21 half Marathon) wakichuana vikali katika mashindano ya mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) katika barabara Bagamoyo jijini Dar es Salaam leo,wakati wa kilele cha mbio hizo kilichofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa mbio za Kilo meta 5 katika mashindano ya Uhuru Marathon akiendele kuchuana.
 Mpiga Picha wa Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) akiendelea kuchukua matukio wakati wa mbio hizo.
 Mgeni Rasmi katika mashindano ya Uhuru Marathon,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha mbio hizo katika Viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania,Suleiman Nyambui akizungumzia mashindano hayo.
Mratibu wa Uhuru Marathon,Innocent Melleck akizungumza machache katika hafla hiyo.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Oscar Shelukindo akiwa na cheti kilichotolewa kwa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa mbio hizo za Uhuru.
 Mgeni Rasmi katika mashindano ya Uhuru Marathon,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21 kwa upande wa wanawake,Catherine Range ambaye amejinyakulia kitita cha sh. mil. 3 za kitanzania.
 Mgeni Rasmi katika mashindano ya Uhuru Marathon,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akimvisha medali kocha wa Mwanariadha Fabian Joseph aliepatwa na dharula ya kimatibabu na kupelekwa hospital mara baara ya kushinda mbio hizo.
 Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment