Friday, November 28, 2014

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA WILAYA YA TANDAHIMBA.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
 Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Juma Njwayo akihutubia wakazi wa Tandahimba mjini ambapo alielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 unavyoendelea jimboni kwake.
 Wanakwaya wa kikundi cha Nia Moja cha Tandahimba wakiimba wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika Tandahimba ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kuimarisha na kukijenga Chama.
 Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
Mjumbe wa kuteuliwa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tandahimba Jaffary Hassan Mwadili almrufu Mwarobaini akiwasalimu wananchi .
Mwarobaini alikuwa  Katibu wa  Chadema wilaya ya Tandahimba baadae akajiunga na CCM
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi kwenye mkutano wa CCM Tandahimba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidia kubeba gunia la korosho kwenye ghala la korosho la TANECU ,Tandahimba mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita juu ya magunia ya Korosho alipotembelea ghala la korosho la TANECU ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama mkoani Mtwara .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya nyumbailiyoezuliwa paa na mvua yenye upepo mkali iliyonyesha jana jioni katika Kata ya Nanyanga Ndugu Saidi Mnambenga ambaye  ni mlemavu wa macho.
 Paa la nyumba ya Ndugu Abdala Athumani Mwatama likiwa chini baada ya kuezuliwa na upepo mkali jana jioni katika kata ya Nanyanga.

 Moja ya nyumba iliyoathirika na mvua za upepo katika kata ya Nanyanga wilaya ya Tandahimba ambapo nyumba zaidi ya arobaini zimeathirika na mvua hiyo

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha lundo la kadi zilizorudishwa kutoka vyama vya upinzani katika kata ya Mahuta wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa Chingongola.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani Tandahimba.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM akiwataka wananchi wa kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwani kura ndio haki yao ya msingi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mahuta huku akiwa ameshikilia kadi za wanachama wa upinzani waliorejea CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mahuta baada ya kufungua shuna la wakereketwa waendesha boda boda Mahuta wilaya ya Tandahimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tandahimba, uliofanyika Mahuta wilayani Tandahimba,Mtwara.

No comments:

Post a Comment