Saturday, November 8, 2014

TASAF YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA TAIFA KUHUSU TUKIO LA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI UKUMBI WA TEC DSM

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16. Wengine (walioketi) ni Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura (wa pili kushoto), meneja masijala ya walengwa Philipine Mmari (wa kwanza kushoto), Mtaalamu wa Mafunzo Mercy Mandawa (wa pili kulia) na Meneja Rasilimali watu Tecla Makundi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiri wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini.
 Afisa Ufuatiliaji na tathmini wa TASAF Bw. Paul Luchemba akitoa mada juu ya malengo ya warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini katika ukumbi wa AMECEA Kurasini Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini  PSSN wakifuatilia mjadala baada ya uwasilishaji wa madajuu ya mwongozo wa mpango katika ukumbi wa TEC-Kurasini jijini DSM
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN wakifuatilia maelekezo toka kwa wawezeshaji.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini  unaotekelezwa na TASAF wakisikiliza mada zinazowasilishwa na wawezeshaji wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa TEC jijini DSM. .
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa neno la ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa (hawapo pichani) kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16 nchini . Aliyekaa kushoto ni  Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura.


TASAF YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA TAIFA KUHUSU TUKIO LA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI UKUMBI WA TEC DSM


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeendesha mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kufanyika kuanzia  Novemba 10 katika halmashauri 16 nchini.

Akifungua  Warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga amesisitiza kuwa suala la nidhamu,uaminifu ,kujituma na kuzingatia taratibu kuwa silaha muhimu katika ufanikishaji wa  utekelezaji wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  ambao umeanza kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.




Bw. Mwamanga ametoa msisitizo huo wakati akifungua warsha ya siku moja ya mafunzo hayo katika ukumbi wa TEC jijini Dar es Salaam ambako amebainisha mambo muhimu yanayochangia  TASAF kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utekelezaji wa shughuli zake ukiwemo utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi ambapo amesema kuwa nguzo kuu ni uwajibikaji wa pamoja na kuzingatia taratbu za Mpango.

No comments:

Post a Comment