Monday, November 3, 2014

6TH ANNUAL JULIUS KAMBARAGE NYERERE COMMEMORATION CAPITOL HEGHTS, MARYLAND

Wasanii Luci Marphy Mmarekani (kushoto) na Anna Mwalagho kuoka Kenya wakiimba wimbo wa Taifa.
Bwana na Bibi Rick Tingling wakiwashukuru watu kwa kuja kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo hiyo jana siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 ilikua ni kumbukumbu ya 6 tangia bwn. Rick Tingling alipoanzisha kumbukumbu za Mwalimu Nyerere mwaka 2009 hapa DMV. Yeye bwn. Tingling ni Mmarekani aliyemjua Mwalimu Nyerere kwa kusoma vitabu vyake na kuanza kumfuatilia na kutambua kwamba Mwalimu Julius Nyerere ni kiongozi asiyekua na mfano na ambaye huwezi kumlinganisha na kionozi yeyeyote hapa Dunia si zama hizo au wakati huu tulio nao sasa. Bwn. Rick Tingling amesema ataendelea kumenzi Mwalimu Julius Nyerere kila mwaka.
Dr. John Rutayuga ambaye ni CEO wa Ukimwi Orphans Assistance akielezea kazi ya kikundi hicho inayofanya nchini Tanzania na baadae kuelezea kuhusu Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii wa mashairi Anna Mwalagho kutoka Kenya ambaye ni mkaazi wa DMV akitoa shairi la I have a dream lililoelezea utajiri wa Africa na kwamba ndoto yake siku moja ni Africa itakua moja na itaitwa United State of Africa.
Mama Elvira William ambaye ni mkurugenzi mkuu wa AHEAD wanaosaidia maswala ya afya na elimu nchini Tanzania tangia mwaka 1974 wakati mume wake Baba Felton William alipoambwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwenda Tanzania kuasaidia maswala ya afya katika hospiali ya Bugando baada ya miaka 2 na nusu walirudi Marekani na mwaka 1985 walirejea tena Tanzania kwa mwaliko wa aliyekua Waziri wa Afya Mhe. Chiduo na kufanya kazi za afya Shinyanga.huku mama William akisaidia kufundisha katika vijiji mkoani Shinyanga. Mwaka 2002 walirudi tena Tanzania na kwa sasa wapo Kisarawe wakiendelea kuasadia katika nyanja ya afya na elimu. Mama William baada ya kueleza kazi zake anazofanya Tanzania alimalizia kw kusoma wasifu wa  Mwalimu Julius Nyerere 
Bwn. Melvin Deal akifanya tambiko kabla ya kuanza kwa kukmbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kulia ni Baba C maarufu kama msimulizi wa hadithi.

Bwn. Melvin Deal ambaye ni m mpiga ngoma wa siku nyingi akielezea maana ya tambiko ambalo baadae alilifanya ukumbini hapo kama ilivyokua likifanywa na mababu zetu enzi hizo.

No comments:

Post a Comment