Monday, October 27, 2014

WAZIRI KAWAMBWA AWA "LAIGWANANI" ACHANGISHA MILIONI 35 UKARABATI WA SHULE YA ENABOISHU MKOANI ARUSHA

 .Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa(kulia)akikabidhiwa Usinga unaomtambulisha kama mzee wa jamii ya Kimaasai(Laigwanani) na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi  ya Kaskazini Kati mkoani Arusha,Solomon Masangwa wakati wa harambee ya kuchangia  ukarabati wa Miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya Enaboishu,Shule hiyo imeanzishwa miaka  48 iliyopita na KKKT.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba yake wakati wa  harambee ya kuchangia  ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Enaboishu,kushoto ni Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa,Mkuu wa Shule hiyo,Lesion Ole Sekioni na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye ni mhitimu wa Shule hiyo,Elisante Ole Gabriel.
 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Maswangwa akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel aliyebuni mpango wa kuwakutanisha wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuchangia maendeleo ya elimu,yeye akiwa mmoja wao.

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Wafanyakazi wa Shule ya Enaboishu
 Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo wakifatilia kwa makini harambee ya kuchangia maendeleo ya Shule ya Sekondari Enaboishu mkoani Arusha.
 Waimbaji wa Empowered Girls Club wakitoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
 Waimbaji wa Empowered Girls Club wakifurahia kitita cha Sh.200,000 walizopewa na mgeni rasmi,Waziri wa Elimu,Dk Shukuru Kawambwa kwa kutoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akipongenzwa na  wanafunzi  wa Shule ya hiyo baada ya kufanikisha harambee .

No comments:

Post a Comment