Wednesday, October 22, 2014

Waziri Kawambwa afanya ziara Mkoani Morogoro

Picha na Habari Na John Nditi, Morogoro

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Morogoro iliyaonza  Oktoba 20 na kufikia tamati  22, 2014

Katika ziara hiyo ya kikazi, waziri baada ya kupkea taarifa ya hali ya elimu mkoa, alitembelea Shule ya  Kilakala Sekondari ya wasichana wa vipaji maalumu kwa ajili ya kupata taarifa za elimu na kukagua miundombinu ya shule.

Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya elimu, pia alikitembelea Chuo cha Ualimu Morogoro , ambapo nako alipokea taarifa ya Chuo na kukagua miundombinu ya Chuo hicho.

Ziara ya Waziri huyo imefikisha pia katika wilaya ya Mvomero ,ambapo alitembelea Shule ya Sekondari ya Kata Kipera ambayo ilipewa fedha na serikali za ujenzi wa nyumba ya mwalimu na maabara ambazo zimekamilishwa.

Mbali na Shule ya Kipera, Waziri huyo aliitembelea Shule kongwe la Sekondari Mzumbe , ambapo alipatiwa taarifa na kukagua miundombinu ya shule , pia aliitembelea Shule ya sekondari Mvomero kukagua ujenzi wa maabara na madarasa ya 'A' Level .

Hata hivyo Waziri huyo licha ya kutembelea shule za sekondari, alipata fursa ya kuitembelea shule ya msingi Manyinga 'A' na kupokea taarifa ya shule hiyo , ambapo pia alikiteembelea Chuo cha Ualimu Mhonda  akiwa na lengo la kupata taarifa na kukagua miundombinu ya Chuo hicho.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Kawambwa, katika ziara hiyo ya siku tatu, ilimfikisha pia Wilaya ya Kilosa, ambapo baada ya kupokea taarifa ya elimu ya wilaya , aliitembelea shule ya msingi Mazinyungu ili kukagua miundombinu ya shule hiyo.

Pia shule nyingine za sekondari alizozitembelea wilayani humo ni ya Rudewa na Kilosa Sekondari , ambapo pia alipata fursa ya kukitembelea Chuo cha Ualimu Ilonga kwa lengo la kupata taarifa ya maendeleo ya elimu na  hali ya miundombinu ya chuo.
Ukaguzi wa majengo ya shule.
Waziri Dk. Kawambwa (suti nyeusi) akipata maelezo ya matumizi ya mkaa rafiki unaotengenezwa na pumba za mpunga na vumbi la mbao na kupunguza gharama ya matumizi ya gesi na kuni kwa huduma za chakula shuleni hapo.
Waziri Dk. Kawambwa (suti) akisikiliza maenezo ya Mwalimu wa Somo la Fizikia walipotembelea maabara ya somo hilo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa ( suti nyeusi kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari KilaKala ya Wasichana wa Vipaji Maalumu , Tabitha Tusekelege, wakati Waziri huyo akitoka kuangalia vyumba vya maabara ya Kemia, Fikizikia na Baolojia na majengo mengine yaliyopo Shuleni hapo Oktoba 20, 2014, alipofanya ziara na kuzungumza na wanajumuiya ya Shule hiyo.
Baadhi ya viumbe mfu na dawa za kimaabara zikiwa zimehifadhiwa chumba kwenye maabara ya somo la Baolojia.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kilakala ya wasichana wa vipaji maalumu iliyipo mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Elimu Dk. Kawambwa (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment