Friday, October 17, 2014

STAND UNITED WATUA BUKOBA! WAFANYA MAZOEZI KAITABA TAYARI KWA KUUMANA NA KAGERA SUGAR KESHO JUMAMOSI

Na Faustine Ruta, Bukoba
Jumla ya wachezaji 26 wa Timu ya Stand United waliotua Mjini Bukoba Jana kwa ajili ya Kipute cha Ligi kuu Vodacom msimu wa 2014-15 na Wenyeji wao Kagera Sugar wamefanya mazoezi yao kwa mara ya kwanza Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba.Wachezaji hao 26 wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na Viongozi wengine 6. Timu ya Stand United ya Shinyanga ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi na kesho Jumamosi inataka Kuibana Timu ya Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wao ambao pia wanashikilia nafasi ya sita kwenye Ligi hiyo ya Vodacom kwa msimu huu ulioanza hivi karibuni. Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Kagera wanaingia wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 4 huku Stand United wakiwa nafasi ya 8 nao wakiwa wanalingana pointi na Kagaera Sugar.Wachezaji wa Stand United wakifanya mazoezi yao ya Mwisho kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini tayari kwa kuumana na Wenyeji wao Kagera Sugar kesho Jumamosi tarehe 18, 2014.Stand UnitedWachezaji wa Stand United wakifanya mazoezi Stand United wakipasha tayari kwa kipute na Kagera SugarVijana wa Timu ya Stand United ya Mjini Shinyanga wakijifua kwenye Uwanja wa Kaitaba leo Ijumaa tayari kwa mtanange wao na Kagera hapo Kesho jumamosi.Kocha Mkuu wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe (kushoto) akiwacheki Vijana wake Wakijifua kwenye Uwanja wa Kaitaba leo Ijumaa Jioni. Kocha Mkuu wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe akisimamia kazi yake ya Ukocha kwenye Uwanja wa Kaitaba leo. Kesho tunataka Ushindi tuu!!Kocha akiteta na Wachezaji wake

No comments:

Post a Comment