Thursday, October 9, 2014

Serikali yaweka Mkakati kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa Wizaraya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.Kushoto ni ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua na wa mwisho kulia ni Mwakilishi wa UNFPA Tausi Hassan.

 Baadhi ya Vikundi vya Burudani wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.
 Baadhi ya wadau wa wiki ya Vijana wakifuatilia Burudani kutoka kwa Kikundi cha JKT hakipo pichani jana mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.


 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akielezea jambo alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa kuwajengea uwezo Vijana kujitengenezea makampuni yao na kumiliki Biashara  alipotembelea banda la Kampuni ya GODTEC jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akiweka saini katika kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa afya zao katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya jana mkoani Tabora ambapo maadhimisho ya wiki ya Vijana yanaenedele.


Na Jonas Kamaleki - MAELEZO

Serikali yaweka Mkakati kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mkakati kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kutenga fedha katika halmashauri mbali mbali nchini kwa lengo la kusaidia miradi ya vijana.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bibi Fatma Mwassa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Vijana mjini Tabora leo (jana). Bibi Fatuma amesema kuwa Mkoa wa Tabora umetenga jumla ya shilingi 1.8 kwa ajili ya kusaidia miradi ya vijana.

“Serikali inatambua changamoto zinazo wakabili vijana ikiwemo ukosefu wa ajira ata hivyo tumekuwa tukijitahidi kukabiliana nazo ikiwemo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia vijana ambapo hapa mkoani kwetu jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetengwa katiak halmashauri zote.” Alisema Bibi. Fatma. Aidha Bibi Fatma aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kusaidia Vijana katika kuendeleza shughuli zao na kuwataka kuwa wabunifu na wenye dhamira ya kweli katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wasitumiwe tu na watu wasioitakia mema nchi bali wajitambue ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuacha tabia ya kukaa vijiweni. Pia amewaasa vijana kutojihusisha na mada ya kulevya. “Msitumike katika kubeba madawa hayo matumboni mwenu au kuyauza reja reja,kataeni kutumikishwa,” alisisitiza Bibi Fatma Mwassa. 

Amewataka vijana watumie fursa zilizopo ili waweze kujiendeleza badala ya kulalamika. Amewaasa watumie ujana wao vizuri kama alivyoutumia Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere ambaye tunaadhimisha miaka 15 ya kifo chake. Alisema Mwalimu aliutumia ujana wake vizuri katika shughuli za kisiasa na kujipatia heshima kubwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Wiki ya Vijana imekuwa jukwaa muhimu kwa Vijana wengi hapa nchini kwani upata fursa ya kukutana na kujifunza kupitia maonyesho yanayoambatanana maadhimisho hayo.

Bibi. Sihaba aliongeza kuwa kumekuwapo na matokeo chanya yanayotokana na maadhimisho hayo ambapo baadhi ya vijana wenye dhamira wemepata kuwa wajasiriamali kupitia wa kubwa na wakati kupitia maadhimisho hayo.

Wiki ya Vijana inaadhimishwa ikiwa inatimizwa umri wa miaka 15 tokea ilipoanzishwa mnamo mwaka 2000 Mkoani Kilimanjaro. Katika Wiki hii Vijana mbalimbali ujumuika pamoja katika maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yanafanyoika mkoani Tabora na yatafikia kilele chake tarehe 14 Oktoba ambayo ni siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele cha mbio za Mwenge.
   

No comments:

Post a Comment