Friday, October 3, 2014

SEMINA YA FURSA 2014 ,JITATHIMINI,JIAMINI,JIONGEZE YAFANYIKA MJINI SINGIDA LEO

 Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Baadhi ya watoa mada mbalimbali katika semina hiyo wakiwa meza kuu
 Baadhi ya Vijana walioitumia Fursa ya kutengeneza fulana za tamasha la Fiesta baada ya kubaini kuna uhaba mkubwa wa fulana hizo,ambazo zilitarajiwa kusambazwa na waandaji wenyewe,Vijana hao waliuza fulana hizo kila moja kwa shilingi Elfu kumi kwa kila moja.
  Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa wamenyoosha mikono juu wakiunga mkono moja ya mada iliyokuwa ikizungumza kwenye semina hiyo iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Muonekano wa ukumbi mlimofanyika semina ya Fursa 2014 mapema leo asubuhi.
 Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka kundi la Hip hop lijulikanalo kwa jina la WEUSI,Niki wa Pili akizungumza mbele ya mamia ya washiriki wa semina ya fursa iliyofanyika katika hoteli ya KBH nje kidogo ya mjini wa Singida,Niki amewataka vijana mbalimbali kuhakikisha ndoto zao haziishii njiani na badala yake wazifanyiekazi ili kujiletea maendeleo katika maisha yao ya kila siku,pia amewataka kuitumia vyema fursa wanayoipata katika njia mbalimbali.v
 Mmoja wa washiriki wa semina ya Fursa,akiulaza swali na pia kuielezea fursa aliyonayo katika harakati za kutafuta maendeleo.
Mkurugenzi wa kampuni ya  Automobile Garage,Joseph Msuya akifafanua jambo kuhusiana na namna alivyoaianzisha kampuni yake na kufikia hapo alipo,akitumia teknolojia za kisasa kabisa katika suala zima la ufundi wa magari,utengenezaji Viyoyozi vya magari na mambo mengine mbalimbali.
  Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa.
 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani),wa semina ya Fursa iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida,ambapo watu mbalimbali wakiwemo wanavyuo walishiriki.
 Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora
 Msanii wa Bongofleva Baba Levo,ambaye pia ni mmoja wa mabalozi wa shirika hilo la NSSF,akielezea yeye na wasanii wenzake wanavyonufaika na fursa mbalimbali zipatikanazo na shirika,Baba Levo amewataka wasanii mbalimbali ambao bado hawajajiunga na shirika hilo wakiwemo na vijana mbalimbali wafanye hivyo sasa,kwani shiriki hilo linatoa fursa nyingi za kuwawezesha vijana kuwapa wigo mkubwa wa kutimiza ndoto za maisha yao
 Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida. 

No comments:

Post a Comment