Tuesday, October 7, 2014

NHC katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Makazi Duniani

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani. Katika ujumbe wake wa siku ya makazi mwaka huu Waziri Tibaijuka ameviagiza vyombo vinavyohusika na upangaji miji kuongeza zaidi kazi ya upimaji wa makazi na kisha kuyaboresha makazi yaliyokwishavurugika kwa hivi sasa kwa mujibu wa takwimu za UN HABITAT, robo ya idadi ya watu wanaoishi mijini kote duniani na Tanzania ikiwamo wanaishi katika mitaa duni ambayo yana mazingira hatarishi, huku hali ya maisha ikiwa yenye uhaba wa huduma muhimu, ujumbe wa mwaka huu ni "Sauti kutoka Makazi Duni"
Waziri Tibaijuka ameziagiza Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya kujenga nyumba angalau 100 kwaajili ya wafanyakazi wake ili kwanza kupanga mij, lakini pia kupunguza tatizo la makazi holela yanayoikabili nchi kwa sasa. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Baadhi ya washiriki waliofika katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa wakipata maelekezo namna nyumba za Shirika zinavyopatikana.
Baadhi ya washiriki waliofika katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa wakipata maelekezo namna nyumba za Shirika zinavyopatikana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa Watendaji wa Shirika la Maendeleo Kigamboni (KDA)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akiwa amewasili katika ukumbi wa mikutano tayari ya kuendelea na shughuli za maadhmisho ya siku hiyo ya kimataifa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akiwa amewasili katika ukumbi wa mikutano tayari ya kuendelea na shughuli za maadhmisho ya siku hiyo ya kimataifa.
Mwakilishi wa Shirika la Makazi laUmoja wa Mataifa (UN HABITAT) Philimon Mutashibirwa akiwasilisha ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi ya wanadamu, UN-Habitat leo mchana.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Subira Sinda akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alimkaribisha Waziri Tibaijuka kuzungumza.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akitoa salamu zake za mwaka za siku ya makazi duniani ambapo aliviagiza vyombo vinavyohusika na upangaji miji kuongeza zaidi kazi ya upimaji wa makazi na kisha kuyaboresha makazi yaliyokwishavurugika kwa hivi sasa kwa mujibu wa takwimu za UN HABITAT, robo ya idadi ya watu wanaoishi mijini kote duniani na Tanzania ikiwamo wanaishi katika mitaa duni ambayo yana mazingira hatarishi, huku hali ya maisha ikiwa yenye uhaba wa huduma muhimu, ujumbe wa mwaka huu ni "Sauti kutoka Makazi Duni"
Waziri Tibaijuka ameziagiza Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya kujenga nyumba angalau 100 kwaajili ya wafanyakazi wake ili kwanza kupanga mij, lakini pia kupunguza tatizo la makazi holela yanayoikabili nchi kwa sasa.
Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Pius Tesha akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofikia kilele chake leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akisikiliza maelezo yaliyotolewa na Afisa wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (National Housing and Building Research Agency – NHBRA) juu ya ufyatuaji wa matofali ya kufungamana kwenye kilele cha maadhimisho ya siku hiyo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akionyeshwa na Afisa wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (National Housing and Building Research Agency – NHBRA) namna matofali ya kufungamana yanavyofyatuliwa
Baadhi ya washiriki waliofika katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa wakipata maelekezo namna nyumba za Shirika zinavyopatikana.
Kikundi cha sanaa na burudani kilivyokuwa kikijimwaya na kutoa ujumbe wao kuhusiana na siku ya makazi Duniani leo mchana
Baadhi ya wajumbe waliofika kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya makazi duniani leo mchana yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “"Sauti kutoka Makazi Duni"”. kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana

No comments:

Post a Comment