Tuesday, October 7, 2014

JK ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI, MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NSSF KIJICHI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea ujenzi wa Daraja la Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea kadi maalum ya pongezi ya siku yake ya kuzaliwa leo Oktoba 07,2014 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau.Rais Kikwete anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo,akiwa ametimiza miaka 64 toka kuzaliwa kwake.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangaliwa maendeleo ya ujenzi wa Daraja Kigamboni jijini Dar es Saalam leo,wakati alipotembelea kuona maendeleo yake.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alieambatana na Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakitembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.ujenzi huo unafanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutembelea eneo hilo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali,Viongozi wa NSSF pamoja na wakandarasi wanaojenga daraja hilo mara baada ya kumaliza kutembelea eneo la mradi huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa NSSF pamoja na wajenzi wa Nyumba za Makazi za shirika hilo zinazojengwa Mtoni Kijichi,jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba za Makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam,wakati alipotembelea kujionea Maendeleo ya mradi huo leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akikata utepe kwenye jiwe la mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mtoni Kijichi,jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau alipokuwa akimfafanulia jambo kuhusu mradi huo wa Nyumba.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.

No comments:

Post a Comment