Saturday, October 4, 2014

BALOZI SEFUE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA DICOTA MJINI DURHAM, MAREKANI

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua rasmi Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. Washiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Watanzania kutoka Majimbo mbalimbali ya Marekani, Wajumbe kutoka Serikalini na Sekta Binafsi na Serikali ya Marekani. Katika hotuba yake ya ufunguzi Balozi Sefue alilipongeza Baraza la DICOTA kwa juhudi na mafanikio mbalimbali na pia alisema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula (mwenye scarf) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Mwalimu Christopher Mwakasege na Wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Alphayo Kidata (wa kwanza kushoto) pamoja na wajumbe wengine akiwemoo Dkt. Joe Masawe (wa kwanza kulia) kutoka Benki Kuu ya Tanzania wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Meya wa Mji wa Durham, Mhe. William Bell akiwakaribisha Wajumbe wa Mkutano wa DCOTA 2014 mjini hapo wakati wa sherehe za ufunguzi
Meya wa Durham Mhe. Bell akimkabidhi Balozi Sefue Cheti Maalum cha kuitambua DICOTA mjini Durham.
Rais wa DICOTA, Dkt. Ndaga Mwakabuta nae akikaribisha Wajumbe kwenye ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Mwaka wa DICOTA 2014
Wajumbe kwenye mkutano wakifuatilia matukio
Sehemu nyingine ya Wajumbe kwenye mkutano
Wajumbe wengine akiwemo Bi. Susan Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Wajumbe mbalimbali kwenye ufunguzi wa mkutano
Mkutano ukiendelea na wajumbe wakifuatilia
Sehemu ya Wajumbe wakijadiliana jambo
Wajumbe zaidi kutoka Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Balozi Sefue akishangiliwa na kina mama wa DICOTA waliokuwa wamevalia sare kumkaribisha kufungua mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Sefue akizungumza na Meya wa Durham, Mhe. Bell
Kina mama wa DICOTA wakati wa shamrashamra za ufunguzi wa mkutano
Balozi Sefue, Balozi Mulamula, Mama Jairo, Mwalimu Mwakasege na Wajumbe wengine wakifurahia nyimbo kutoka kwa kina Mama wa DICOTA kabla hala ya ufunguzi haijaanza.
Kijana wa DICOTA, John Mmanywa akiimba kwa ufasaha kabisa Wimbo wa Taifa la Tanzania.

----------Matukio kabla ya ufunguzi wa Baraza la DICOTA

Balozi Sefue akipata maelezo kutoka kwa Mjumbe kutoka Benki ya CRDB kuhusu huduma yao ya Tanzanite Account maalum kwa Diaspora. Kulia ni Dkt. Sweetbert Mkama kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Sefue akiendelea kupata maelezo katika meza za maonesho ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya Diaspora na nchi
Balozi Mulamula akisalimiana na Mwalimu Mwakasege huku Balozi Sefue akishuhudia.
Balozi Sefue katika picha ya pamoja na Mwalimu Mwakasege
Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na Bibi Jairo
 Msanii wa vichekesho Masanja Mkandamizaji akisalimia wadau kwa kuwavunja mbavu kwenye DICOTA 2014 Gala Dinner iliyofanyika Ijumaa usiku Oct 3, 2014 katika Hotel ya Millennium Durham, North Carolina nchini Marekani kwenye Gala Dinner kulitolewa vyeti kwa wadhamini wa ndani na nje ya Marekani waliowezesha DICOTA 2014 Convention kuwa ya mafanikio.

Waliowezesha DICOTA 2014 Convention kupata mafanikio kuanzia uongozi wa juu wa DICOTA mpaka kamati ya maandalizi wakaazi wa North Carolina wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Bw. Alphayo Kidata, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mkuu wa kitengo cha Disapora Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Rosemery Jairo
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea machche kuwashukuru Viongozi wa DICOTA na kamati nzima ya maandalizi kwa kuwezesha kufanikisha DICOTA 2014 Convention na kuwaasa daima wawe na malengo ya kuangalia mbele na kuweza kumkomboa mwanadiaspora katika katika nyanja mbalimbali za maendeleo na hatimae mwanadiaspota atumie  ujuzi na ufanisi wa maendeleo hayo kusaidia nyumbani.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea machche na kutoa shukurani zake kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa kukubali kuja na kuendelea kuwa na Imani na DICOTA pia alipata nafasi ya kuwashukuru wadhamini toka Tanzania bila kumsahau mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rosemery Jairo.

Katika Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakibadilishana mawili matatu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwenye DICOTA 2014 Convention Gala Dinner.
Mkuu wa kitengo cha Disapora Bi. Rosemery Jairo akiwa katika picha na Dr. Samakula.
 
Juu na chini ni Fashion show kwenye gaka dinner ya Dicota 2014 Convention
 Juu na chini fashion show ya Kwetu fashions by Missy Temeke

Juu na chini ni utoaji vyeti kwa wadhamini wa DICOTA 2014 Convention
Juu na chini ni uotoaji vyeti na tuzo kwa washindi wa DICOTA 2014 Convention kwa wadau wa diaspora katika nyanja tofauti.
 Washindi wa tuzo katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

No comments:

Post a Comment