Tuesday, October 21, 2014

Airtel yazindua wiki ya Rasilimali watu kwa wafanyakazi wake

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi wiki ya Rasilimali watu itakayowawezesha wafanyakazi wake kupata elimu kuhusu Sera na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wafanyakazi na kusimamiwa na kitengo cha Rasillimali watu kwa lengo la kuwaongezea wafanyakazi ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja.

Airtel imeandaa wiki hiyo ya rasilimali watu katika nchini zote Afrika ambapo Airtel inafanya biashara zake na kuzinduliwa rasmi leo nchi Tanzania, airtel imefanya hivyo leo ikiwa ni muda mfupi tu tangu ilipoadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa duniani kote ambapo airtel ilishiriki katika maadhimisho hayo .

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa kitengo cha Rasilimali watu Bwana Patrick Foya alisema” Tunategemea kuwa na wiki yenye mafanikio ambayo itawawezesha wafanyakazi wetu kupata ufafanuzi juu ya maswala mbalimbali yanayohusu sera na haki zao za msingi kama wafanyakazi wa Airtel.

Sambamba na hilo tutakuwa na watoa huduma kutoka kwenye makampuni mengine wakiwemo strategies inayotoa huduma za bima ya afya, NSSF inayotoa mikopo ya nyumba na mafao kwa wafanyakazi na makapuni mengine mengi ambayo yatatoa fulsa ya wafanyakazi wetu kupata elimu zaidi kuhusu huduma hizi muhimu na jinsi yakufaidika nazo hii ni fulsa kwa wafanyakazi wetu nasi tuko tayari kuwafikishia wote ili kuongeza ufanisi kazini".

Natoa wito kwa wafanyakazi kujitokeza katika sehemu maalumu zilizoandaliwa kutoa huduma na kupata mambo mazuri tuliyowaandalia wiki nzima alingoza Foya.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwashukuru wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu kwa kujipanga vyema kwa wiki hii na kusisitiza kuwa elimu na mafunzo haya ni mwendelezo wa mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa wafanya kazi wote wanajua mambo muhimu yanayotokana na ajira zao, sera mbalimbali kama vile za afya na zile zinazogusa maslahi yao'.

Colaso alisema “ natoa wito kwa wafanyakazi kutumia wiki vyema na kuuliza mswali mengi yatakayo toa ufafanuzi wa maswala wanayohitaji elimu na uelewa zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwn Sunil Colaso akiongea na wafanyazi wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu cha Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam.

wafanyakazi wa Airtel wakifatilia uzinduzi wa uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam
Meneja Rasilimali watu Airtel Bi Sophia Melamari akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali watu Airtel Tanzania Patric Foya akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.

Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu kama MC Pilipili akitoa burdani kwa wafanyakazi wa Airtel wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.
Wafanyakazi wa Airtel wakifurahia burdani toka kwa Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu kama MC Pilipili wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.


No comments:

Post a Comment