Wednesday, September 10, 2014

VODACOM YAMWAGA VIFAA VYA TIMU 14 ZA LIGI KUU

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim,akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom. kushoto ni Meneja biashara wa TFF Peter Simon na kulia ni Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga.Timu 14 zimekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh 430 Milioni.
Kutoka kushoto: Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Silas Mwakibinga,Mwakilishi wa klabu ya Azam FC Phillip Alanzo na Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakionesha jezi za Azam FC walizokabidhiwa na mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom kampuni ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2014/2015. Timu 14 zimekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh 430 Milioni.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto) akimkabidhi jezi Mwakilishi wa JKT Ruvu akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga(katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.Vifaa hivyo zimetolewa na wadhamini w aligi hiyo kampuni ya Vodacom.
Kutoka kushoto: Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga,Mwakilishi wa timu ya Kagera Sugar na Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakionesha jezi ilziokabidhiwa timu ya Kagera kwa na kampuni ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2014/2015. Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo.
Mwakilishi wa timuu ya Mbeya City akipokea kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto) jezi zitakazotumiwa na timu hiyo katika msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu ya Vodacom. Wa pili toka kusho ni Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange .Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14 zitakazoshiriki ligi kuu vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 430.
Mwakilishi wa Timu ya Simba akipokea kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto) jezi zitakazotumiwa na timu hiyo katika msimu huu mpya utakaoanza hivi karibuni. pili toka kusho ni Afisa mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange. Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14 zitakazoshiriki ligi kuu vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 430.
Kutoka kushoto Meneja Biashara wa TFF Peter Simon, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga na Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakifurahia jambo pamoja na Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto wanne toka kushoto wakati wa hafla ya Vodacom kukabidhi vifaa kwa timu 14 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Silas Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakifurahia jambo pamoja na Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto wane toka kushoto wakati wa hafla ya Vodacom kukabidhi vifaa kwa timu 14 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
AfisaMendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga(katikati)akipokea vifaa vipya toka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, vitakavyotumiwa na waamuzi katika mechi mbalimbali za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazoanza hivi karibuni. Jumla ya zaidi ya shilingi Milioni 430 zimetumika katika kununua vifaa kwa timu 14 zitakazoshirikii Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 pamoja na vifaa vya waamuzi.

No comments:

Post a Comment