Monday, September 29, 2014

KUNDI LA WAMAREKANI WAJA NCHINI KUTIZAMA FURSA ZA UWEKEZAJI

Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji.
Afisa Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya  Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi.
Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc  ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Mount Meru, jijini Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa tayari ambaye ni ziara yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza uwekezaji katika sekta ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii Carfonia Marekani iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikwete.
Mtaalamu wa Ujenzi wa nyumba za makazi ,Nishati Erick Nyaren akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wao Tanzania .Nyaren yuko nchini kuangalia fursa katika uwekezaji katika sekta ya Ujenzi. na Miundo mbinu.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yao ya siku sita nchini Tanzania ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vya ,Manyara,Serengeti na Ngorongoro.Crowford yuko nchini kutizama fursa ya uwekezaji inayopatikana katika sekta ya Kilimo.
Mhandisi wa vifaa vya matibabu,Bob Reynolds akizungumza na waandishi wa habari namna anavyofikiria kuwekeza katika sekta ya Afya hasa kwa kutizama upatikanaji wa vifaa tiba kama X Ray,Ultrasound na CT Scan.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc wakiwa katika pozi la Picha katika hotel ya Mount Meru.
Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya Marekani wakiwa katika picha ya pamoja katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments:

Post a Comment