Monday, August 11, 2014

TAASISI ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UZAZI


 Kina mama wakionyesha mfano wa kuwanyonyesha watoto wachanga katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa
 Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards akizungumza. (picha zote na Denis Mlowe)
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizundua kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto) ni kaimu mkurugenzi wa mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania Dk. Joyceline Kaganda na katibu tawala mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akionyesha kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo mara baada ya kukizundua rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto)ni katabu tawala mkoa wa Iringa na kulia nimwakilishi wa Unisef tanzania Paul Edwards.
 Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiigiza kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiimba kwa hisia kali kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.

 Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
 Msanii wa marufu nchi Emanuel Mgaya 'Masanja' akiongoza maandamano ya kuadhimisha kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi.

Na Denis Mlowe,Mufindi.

SERIKALI imewataka waajiri katika taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia na kulinda sheria zinazowalinda wanawake wanaojifungua kwa kuwapa likizo za uzazi kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake.
 
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa juzi, mgeni rasmi Katibu wa Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo, mwanamke aliyejifungua mtoto mmoja anatakiwa kupewa likizo ya uzazi ya siku 84 na aliyejifungua watoto mapacha anapewa likizo ya siku 100.
 
Alisema likizo hizo zinaambata na malipo kamili ya mshahara na mama aliyejifungua anaweza kuchukua likizo yake ya mwaka akihitaji na mzazi aliyerudi kazini baada ya likizo ya uzazi anapewa ruhusa ya saa mbili kwa siku kwenda kumnyonyesha mtoto.
 
Pallangyo aliwaasa wadau wengine wanaojishughulisha na uuzaji wa maziwa mbadala ya watoto, mikoa na halmashauri zote kujua na kufuata kanuni za kitaifa zilizotungwa chini ya sheria za mamlaka ya chakula dawa na vipodozi sura ya 219 kudhibiti uuzaji na usambazaji wa maziwa mbadala ya watoto pamoja na bidhaa zinazoambatana na vyakula vya watoto.
 
Aidha alivitaka vyombo vya habari kuelimisha wanafamilia na wanawake hasa wanawake wanaojiita wa kileo ambao wanaiga tamaduni za kigeni za ulishaji watoto ambazo mazingira yake ni potofu.
 
“Tungependa kuwaona hawa wanawake wa kisasa wanabadilika na kuelewa kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto hasa katika miezi sita ya mwanzo ili kuwajengea watoto msingi mzuri kimwilina kiakili hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo kamati za lishe za mikoa na wilaya ili kuhakikisha kwamba elimu inatolewa kwa wanawake wote” alisema Pallangyo
 
Awali Mkuu wa mkoa wa Iringa Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Ayubu Warioba, aliitaka jamii kuelimishana kwenye kaya na jamii kuhusu unyonyeshaji na ulishaji sahihi wa watoto katika ustawi na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema jukumu la kuboresha afya na uhai watoto wa kitanzania ni la wananchi wote likianzia na mtu binafsi na familia kwa ujumla.
 
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards alisema shirika hilo na wadau wengine linalenga kuimarisha unyonyeshaji  wa maziwa ya mama kama njia ya ufanisi na kuokoa maisha ya mtoto.
 
Alisema shirika hilo litawajengea uwezo watoa huduma za afya kwenye vituo na wahudumu wa afya vijijini pamoja na watu wengine ambao ni muhimu katika kufanikisha mipango ya kuboresha lishe kwa watoto


No comments:

Post a Comment