Sunday, August 17, 2014

Serikali kutatua mchangamoto za barabara kuwezesha miradi ya NSSF kufanikiwa

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi. 
 Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kushoto) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
  Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto mbele) akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kushoto mbele) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
 Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (kushoto) akimuonyesha waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) moja ya sehemu za ndani ya mradi wa nyumba wa NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, unaondelea kujengwa, wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofsdhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (watano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa nyumba za NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500 wa nyumba zenye gharama nafuu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.



Serikali imesema itajipanga ili kuona namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali ambazo zitaweza kukwamisha miradi mikubwa yanayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) yatakayo badilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam..

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyasema hayo baadaa ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) amayo ni pamoja na daraja la Kigamboni, mradi wa nyumba za gharama nafuu inayojengwa Mtoni Kijichi na mradi wa nyumba Zaidi ya 7000 uitwao  ‘Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.

Akizungumza wakati wa kukamilisha ziara yake huko Dege Kigamboni katika mradi wa nyumba Zaidi ya 7000 uitwao  ‘Dege Eco Village’ Jumamosi , Pinda alisema Kigamboni inendelea kwa kasi kubwa kiasi kwamba miundombinu iliyopo haitoshi kuhimili idadi ya watu watakaohamia.

“Tunahitaji kujipanga kwa dhati kuhakikisha barabara na vivuko vinafanya kazi. Changamoto kubwa hapa ni barabara za viuongo kutoka Mandela upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni pia. Barabara hivi zote sita za darajani zitatakiwa kufika Kigamboni, Mjimwema, Mbagala na kwingineko,” alisema.

Pinda alisema daraja litakapo kamilika, watumiaji watatozawa tozo la barabara ili kuweza kulihudumia. Alisema serilaki inafikiria pia namna ya kuipanga Kigamboni ili iendane na maendeleo yanayokuja.

 Kuhusu Mradi mkubwa wa Dege Eco Village wenye uwezo wa kuchukua nyumba za gorofa Zaidi ya 7000 na za kawaida (villas) 300, Waziri mkuu alisema mradi huo utaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya taifa kwani hakuna mji utakao fanafana na ule kati ya miji mingi aliyofika.

Aliitaka Manispaa ya Temeke kuangalia idadi ya watu kule Kigamboni  ili serikali iangalie uwezekano wa namna ya kupanga usimamizi kiutawala.

Pinda alifurahishwa na kitendo cha NSSF kuwapa kipaumbele wanachama wake kupata nyumba ambazo zimejengwa katika mradi wa Mfuko huo uliopo Mtoni Kijichi. Tayari nyumba 85 zilizojengwa katika awamu ya kwanza zimeshachukuliwa na wanachama. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Novemba 2008 na kukamilika 2010.

Nyumba 215 zilizojengwa katika awamu ya pili nazo zimeshachukuliwa na wanachama na baadhi ya wadau wengine. Nyumba hizo kwa mujibu wa Meneja Miradi, Mhandisi John Msemo, zilianza kijengwa mwaka 2011 na kumalizika mwaka 2013 ikiwa ni awamu ya tatu.

Mhandisi Msemo alisema awamu ya tatu ndio inaendelea kwa sasa ya ujenzi wa gorofa na nyumba za kawaida (villas) jumla yake ikiwa ni nyuma 820, mradi ambao ulianza mwaka jana 2013 na unatarajiwa kumalizika 2015. Tayari nyumba 300 zimeshalipiwa kabla hazijamalizika.

Akiongea na waandhishi wa habari baada ya ziara ya waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhani Dau alisema miradi yao ilikuwa inapata changamoto kubwa hasa upande wa barabara.

“Tukimaliza ujenzi wa daraja tunategemea barabara zote jijini ziwe zimeisha ili kupunguza msongamano katika daraja. Itakuwa haina maana kumaliza daraja wakati maungio hayajakamilika,” alisema.

Aliongeza pia kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza wa miradi hiyo ikiwemo ya kutopata ardhi toka kwa wananchi kwa muda unaofaa, serikali kuchelewa kutoa asilimia 40 ya sehemu yake katika mradi na pia masuala ya kitaalamu katika ujenzi wa daraja.

Kuhusu mradi wa nyuma Mtoni Kijichi, alisema walikuwa wanahitaji sana daraja litakounganisha Mtoni Kijichi na Mbagala kwani nirahisi sana kuvuka sehemu hiyo na kuingia kigamboni kiurahisi kuliko kutumia Zaidi ya kilometa 20 kuzunguka katika daraja ili mtu afike Kigamboni au Mbagala.


Tatizo la maji alisema walilazimika kuchimba visima wakati DAWASA waki jiandaa kufanya taratibu za kuweka maji.

No comments:

Post a Comment