Saturday, August 2, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YAENDELEA NA UTEKELEZA WA ILANI YA CCM JIMBO LA KAWE

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Jengo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) ambalo linajengwa katika eneo la Mabwepande, likiwa ni sehemu ya Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, walipotembelea kiradi mbalimbali ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015 katika jimbo la Kawe.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuf Mwenda, akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo yeye na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni walipofika kwenye mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Jimbo la Kawe unaofanyika Mambwepande, jana.
 Mwenda (wapili kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) la hospitali ya Jimbo la Kawe inayojengwa Mabwepande, Dar es Salaam.
 Mwenda akiingia ndani ya chumba cha mapokezi cha jengo hilo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) wakati wa ziara hiyo.
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Cholage akiwaonyesha wenzake eneo aliloona kuwa ni kama kasoro kwenye ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye hospitali hiyo.
 Mwenda akifanya majumuisho na wajumbe baada ya kutembelea jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye Hospitali ya jimbo la Kawe inayojengwa mabwepande.

UJENZI WODI YA KINA MAMA NA NYUMBA YA MGANGA ZAHANATI YA NDUMBWI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akiongozwa jana na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndumbwi, Sophia Kasubi, kuingia kwenye jengo la wodi ya Kina mama ambalo ujenzi wake umekamilika kwa ajili ya zahanati hiyo.
 Mwenda akisaini kitabu cha mapokezi kwenye jengo hilo wodi ya Kina mama kwenye zahanati ya Ndumbwi baada ya kuingia yeye na wageni wenzake.
 Mwenda akiongozana na Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni Athumani Sheshe baada ya kukagua nyumba ya mganga kwenye zahanati ya Ndumbwi.
 Mwenda akiagana na watumishi wa zahanati ya Ndumbwi
 Baadhi ya watumishi katika zahanati ya Ndumbwi

UJENZI SHULE YA SEKONDARI KATIKA ENEO LA MIKOCHENI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inajengwa na Manispaa hiyo katika eneo la Mikocheni.
 Mwenda akishiriki ujenzi wa shule hiyo ya sekondari kwa kuchanganya mchanga na saruji wakati wa ziara hiyo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kinondoni Pili Chande akishiriki ujenzi Shule ya Sekondari inayojengwa Mikocheni, jana. Kushoto ni Mwenda akishuhudia na aliyesimama kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi Kata ya Kawe, Eddy Mlaponi
 Mwenda akizungumza na wajumbe kufanya majumuisho baada ya kukagua shule hiyo ya sekondari Mikocheni na kuridhika kwamba ni mradi mzuri unaopaswa kupigiwa mfano katika utekelezaji wa ilani ya CCM

UJENZI SOKO BUNJU 'B'
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa soko katika eneo la Bunju B jana.
 Mmoja wa wajumbe akilazimika kwenda kukagua hali ya choo kwa ajili ya soko hiyo ipoje kwa ajili ya matumizi ya binadamu?
UJENZI DARAJA MIKOCHENZI FEZA
 Wajumbe wakikagua daraja lililojengwa katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika eneo la Mikochezi-FEZA.
Wajumbe wakiwa wameshuka kwenye basi kukagua ujenzi wa barabara ya Maandaazi eneo la Msasani ambayo pia imeboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)


*Yatekeleza agizo la Rais Kikwete
*Ni la jimbo kuwa na hospitali kubwa
 NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeshuhudia makubwa yaliyofanywa na Manispaa ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya jimbo la Kawe.

Miongoni mwa miradi ambayo chama kililazimika kumpongeza Meya wa Manispaa hiyo ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya ujenzi wa Hospitali kubwa katika jimbo la Kawe yenye hadhi kama zilivyo za Mwananyamala, 
Amana na Temeke.

Katika uteekelezaji agizo hilo la Rais Kikwete ambayo haikuwemo katika ilani, tayari Manispaa ya Kinondoni imeshaanza ujenzi wa hospitali hiyo katika eneo la Mabwepande, kwa jengo la kupokea wagonjwa (OPD), linalotarajiwa kukamilika mwaka huu, ambapo imeelezwa hadi mwishogharama yake itakuwa sh. milioni 288 ambazo kati yake sh. milioni Sh.153 zimeshalipwa kwa mkandarasi.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 katika jimbo la Kawe, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, waliokuwa kwenye ziara hiyo jana, walielezwa kwamba, baada ya kukamilika ujenzi wa jengo hilo la kupokea wagonjwa, utaanza ujenzi wa wodi ya kina mama.

"Ndugu wajumbe, wakati Rais Kikwete akiwa katika kampeni zake katika uchaguzi mkuu uliopita, aliagiza kwamba kila jimbo latika mkoa wa Dar es Salaam, lazima liwe na hospitali yenye hadhi kubwa. Sasa ukiangalia agizo hilo ni kama lilikuwa linatulenga sisi wa jimbo la Kawe, maana Jimbo la Kinondoni ipo ya Mwananyamala, Ilala ipo Amana na Temeke pia ipo, ndiyo  sababu tumefanya kila jijitahada kuhakikisha sisi Manispaa tunajenga hospitali hii.", alisema Mwenda.

Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM, wakiendelea na ziara hiyo, pia walishuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya sekondari unaoendelea katika eneo la Mikocheni, unaotekelezwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.5 kwenye awamu ya kwanza.

Mwenda alisema, kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ambayo imekuwa ikiwapata wananchi wa jimbo hilo kwa watoto wao kwenda maeneo ya mbali wanapojiunga na shule ya sekondari baada ya mitihani ya darasa la saba.

Alisema, ujenzi wa shule hiyo ambao sasa upo kwenye hatua ya orofa ya kwanza, unatarajiwa kukamilika mapema na marajio ni kuwezesha watoto watakaomaliza darasa la saba mwaka huu, kuanza kidato cha kwanza kwenye shule hiyo.

Wajumbe hao pia walitembelea mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Bunju B, ambalo ujenzi wake unafanyika ili kuwahamishia wafanyabishara ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo katika eneo hilo la Bunju B na hivyo kuhatarisha maisha yao na pia kuharibu mandhari ya mji.

Ujenzi wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 90, na taratibu za kuanza kuwahamishia hapo wafanyabiashara zinaendelea kufanywa na mamlaka zinazohusika.

Baadhi ya miradi mingine ambayo wajumbe hao waliikagua na kuonyesha kuwasisimua, ni ujenzi wa wodi na kina mama na nyumba ya mganga ambavyo vimekamilika, katika zahanati ya Ndumbwi  kwenye jimbo hilo la Kawe.

Pia alikagua na kuridhiwa na hatua iliyopigwa na Manispaa ya Kinondoni katika ujenzi wa barabara za Maandazi iliyopo Masasani, na barabara ya Jourunalism iliyopo eneo la Feza, Mikocheni.

No comments:

Post a Comment