Sunday, August 24, 2014

MACHAVA FC KUTUMIA UZI MPYA TOKA MEGATRADE KATIKA MECHI YAO DHIDI YA PANONE FC ITAKAYOSHUHUDIWA NA MAGWIJI WA REAL MADRID UWANJA WA USHIRIKA MOSHI

Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa nahodha wa timu ya soka ya Machava fc.
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa mlinda Mlango wa  timu ya soka ya Machava fc
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka (kushoto)akikabidhi msaada wa jezi kwa Makamu mwenyekiti wa timu ya soka ya Machava fc,Abuu Masudi.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha timu ya Machava fc ya mkoani Kilimanjaro wakionesha uzi mpya waliopewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Panone fc uliondaliwa mahususi kwa ajili ya Magwiji wa soka wa klabu ya Real Madrid utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.

MAGWIJI wa klabu ya Real Madrid ya Hispania leo (kesho) wanaendelea na ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa watatembelea lango la kupandia mlima Kilimanjaro la

Marangu.

Katika ziara hiyo ya kitalii chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kimeiteua klabu ya soka inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Panone FC kuwa wenyeji wa magwiji hao ambao pia watashuhudia mchezo wa
kirafiki kati ya timu za Panone fc na Machava fc utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema ofisi yake imeandaa utaratibu wa namna ya kuwapokea magwiji hao pamoja na kuandaa ratiba maalumu ya kutembelea vivutio ukiwemo mlima Kilimanjaro pamoja na
kushuhudia mchezo mmoja wa Kirafiki.

“Katika  tasnia ya michezo nchi yetu  imepata bahati kubwa ya kutembelewa na wachezaji  wa zamani  Real Madrid ambao pamoja na ziara yao wamepanga kutembelea mkoa kwetu ,kikosi hicho kitaingia kati ya saa tano au saa tano na nusu watashuka uwanja wa ndege wa KIA,”alisema
Gama.

Alisema baada ya kupokelewa moja kwa moja magwiji hao watapelekwa Mlima Kilimanjaro katika ofisi za hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA ambako watapata fursa ya kupanda mlima huo kwa hatua chache baada ya kupokea taarifa ya shughuli za utalii kwa ujumla.

“Tumewaandalia sehemu ya kupata chakula cha mchana na wenyeji wao klabu ya Panone fc , baada ya chakula tukasema ni vizuri waone hatupo mbali katika michezo, kwa hiyo tumepanga kuwa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Panone fc na Machava ikitanguliwa na ikitanguliwa na mechi ya vijana chini ya miaka 15 .”alisema Gama.

Gama aliwataka  wadau na wapenzi wa michezo mkoani humo kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika mapokezi makubwa ya wachezaji hao wa zamani na kwamba licha ya kuwa dhamira yao ni kuimarisha utalii lakini pia wangependa kuona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro.

“Ni vizuri wakaona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro na pengine wakapata nafasi ya kuona vipaji vyetu ,mimi ninauhakika hapa kuna wachezaji wanaweza kuchukuliwa na Real Madrid kwa sababu tunaweza
kufanya vizuri sana,,,kwa hiyo niwaombe wanamichezo wetu wajitokeze kwa wingi tukawaone nyota hawa wa Madrid na pengine tuwape ukarimu wetu wa kitanzania tuliouzoea.”alisema Gama.

Kwa upande wao klabu ya soka ya Panone fc kupitia msemaji wake Kassim Mwinyi alisema wamefurahishwa na ujio huo na kwamba klabu imejipanga kujenga mahusiano na magiwji hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu
katika maswala ya michezo.

“Tumepata fursa kama Panone fc  ya kukutana na Magwiji hawa wa Madrid ,sisi tumejipanga kutumia ujio huu katika kujenga mahusiano ya kitimu kati yetu na wao ,na hakika utakuwa ni mwanzo mwema kwa klabu yetu 
ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza”alisema Mwinyi.

Magwiji hao watakao ongozwa na wanasoka waliowahi kutamba katika ulimwengu wa soka kwenye ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga,ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays,michuano ya Mabingwa na ile ya kombe la dunia wakiwa na nchi zao wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya ziara maalumu.

Baadhi ya Wanandinga hao wa zamani waliotamba na Real Madrid kwenye michuano ya La Liga, UEFA pamoja na kombe la dunia wakiwa na nchi zao watakaofanya ziara ya siku nne nchini ni pamoja na Zinedine zidane, Luis Figo, Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima, Christian karembeu na 
Michael Owen.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya kaskazini,

No comments:

Post a Comment