Monday, August 18, 2014

CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO (UB) CHATOA MAFUNZO KWA MAOFISA WA SERIKALI KUTOKA NCHI 15 KUHUSU UANDIKAJI WA MIKATABA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kuhusu uandikaji wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara wakiwa katika majadiliano wakati wa mkutano huo. Washiriki katika mkutano huo wanatoka katika nchi 15 nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Nordic Africa Institute (NAI) kwa kushirikiana na Trans African University Partnership (TANUP/PUTA), pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SiDA) na FAO.zinazoendelea. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakiwa katika majadiliano.
Professa Dickson Yeboah kutoka Shirika la Biashara Duniani (WTO) akitoa mada wakati wa mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kutoka katika nchi 15 za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini kuhusu uandikaji wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara.

 Washiriki wakiwa katika mkutano huo.
 Tunajifunza jinsi ya kuandika mikataba ya Uwekezaji na Biashara.............
 Washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na Viwanda wakiwasili katika  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Washiri hao wanatoka katika Wizara za Uwekezaji na Biashara ambapo washiriki 15 kutoka katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini wanashiriki mkutano huo. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Nordic Africa Institute (NAI) kwa kushirikiana na Trans African University Partnership (TANUP/PUTA), pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SiDA) na FAO.
 Mkurugenzi wa Fedha Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Job Chacha akiwakaribisha washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki  wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, wakisaini kitabu cha wageni walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali ili waweza kupata uwezo wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki  wa mkutano huo.
 Baadhi washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wakimsikiliza Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo walipotembelea  Ofisi za Chuo hichoMikocheni jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wakimsikiliza Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo.
 Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Uchumi na Usimamizi (UB) Dk. Lenny Kasoga na Mkurugenzi wa Fedha UB, Dk. Job Chacha.
 Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoaj na washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment