Monday, August 18, 2014

Benki ya Exim yasheherekea miaka 17 ya utoaji huduma na wateja wake

 
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania na baadhi ya wateja wakionyesha fataki kusheherekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
 Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugene Masawe (wa kwanza kulia) naMeneja Mwandamizi wa Tawi la Samora, Nancy Huggin (wa kwanza kushoto) pamoja na wateja wa benki hiyo wakikata keki kusherehekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997. (Picha na mpiga picha wetu).
Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania (wakwanza kulia) akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997
 Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugen Masawe (Aliyenyanyua mikono) akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
Baadhi ya wafanyakazi wakongwe wa Benki ya Exim Tanzania katika picha ya pamoja iliyopigwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.

IKIJIKITA katika safari yake tangu mwaka 1997 ikiwa na tawi moja na kupanua wigo wake mpaka matawi 27 nchini na nje ya nchi, Benki ya Exim imepiga hatua ya kipekee katika sekta ya kibenki nchini Tanzania. Ikidhiirishwa na miaka 17 ya historia ya Benki iliposheherekewa Ijumaa Agosti tarehe 15 na wafanyakazi wa benki pamoja na wateja nchi nzima. 

Benki ya Exim imekuwa na mpango kazi madhubuti wa 'upanuzi na ugunduzi' tangu kuanzishwa kwake kama benki ya kitanzani, mali zake kwa jumla zikiwazimevuka shilingi tilioni moja ilipofika mwezi Juni 2013.  Bw. Eugene Masawe, Mkuu wa Idara ya Uendeshaji na mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu alisema; "maadhimisho ya miaka 17 ya benki yanaashiria mafanikio makubwa kwa miaka mingi, yaliyodhiirishwa na utendaji wake mzuri wa kuwa na dhamira ya kuwa "benki bora zaidi ya wengine".

Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ya Exim hayaonyeshi tu mafanikio yaliyopatikana katika miaka hiyo lakini pia uongeza hari ya utendaji mzuri kwa wafanyakazi wote. Wakati faida ghafi ya benki ikikua kwa asilimia 80 (shilingi bilioni 9.6), pato la jumla litokanalo na riba likikua asilimia 36 (shilingi bilioni 14.3) na pato kupitia biashara ya fedha za kigeni liliongezeka kwa  asilimia 33 kuanzia mwaka jana ni viashirio thabiti kwamba benki hiyo itafikia malengo katika miaka michache ijayo.

Utendaji huo wenye mafanikio wa Benki ya Exim umetokana jitihada za benki hiyo kutoa huduma za kipekee zikiungwa mkono na wafanyakazi mahiri pamoja na wateja waaminifu na kuifanya benki kuwa ya kwanza katika Huduma kwa Wateja (Customer Care) nchini Tanzania mwaka 2012 (Ripoti ya KPMG).

Ikiwa na zinazomlenga mteja za rejareja, mikopo mbali mbali na kuanzisha huduma za kibenki za kisasa vimekuwa na  umuhimu mkubwa kwa kuendana na kauli mbiu ya benki ya, 'ugunduzi ni maisha.’

Naye Nancy Huggin, Meneja Mwandamizi wa tawi la Samora akasema, "sasa tumejikita katika mpango wa kibunifunifu ujulikanao kama innovative retail model utakao tusaidia kuboresha mawasiliano na wateja na uratibu wa matawi katika maeneo tunayofanyia kazi."

Kwa upande wake, Issa Hamisi, kaimu Afisa wa Fedha Mkuu aliongeza; “kipaumbele chetu kikubwa kinabaki kuendelea kuimarisha nafasi yetu katika soko na kuboresha ufikiwaji wa matakwa ya mteja kupitia utendaji ulio na ufanisi.”

Katika siku hiyo maalum, Benki ya Exim iliwaalika baadhi ya wateja wake kusherehekea maadhimisho hayo katika matawi yote nchini Tanzania kwa wafanyakazi wa jijini Dar es Salaam wakisheherekea katika Tawi la Samora ambapo Benki ya Exim ilizaliwa.

Wakati wa tukio hilo la kukumbukwa, Bw. Masawe aliongeza na kusema, "Baada ya kumaliza miaka 17 ya shughuli zenye mafanikio Tanzania, tutaendelea kusimama imara, na kuendelea na kuwa na mpango wa ukuaji  tukijikita zaidi na utoaji wa huduma zenye ubora zaidi na vile vile bidhaa na huduma zilizo na ubunifu zaidi."

No comments:

Post a Comment