Saturday, July 12, 2014

Ya kuzingatia unapochagua mtoa huduma ya IT Tanzania

Katika maisha ya kiujasiriamali ya sasa, hauwezi kuepuka maumizi ya Tekinolojia.Tekinolojia siyo tu inakuwezesha kufikia watu wengi zaidi, bali pia kuongeza ubora na ufanisi wa huduma zako kitu kitakachokufanya uwe wa kipekee.
Wajasiriamali wengi wamekuwa na shauku na hamu kubwa ya kutumia tekinolojia ili kuongeza ufanisi wa huduma zao. Kwakuwa wengi wa wajasiriamali hawa hawana uelewa mkubwa wa mambo ya tekinolojia (na si kazi yao), hivyo hujitoa kafara kwa watu wa tekinolojia wakiamini wao ndiyo msaada wao mkubwa. Lakini si mara zote mambo yanaenda sawa.
Tangu kuanzishwa kwa Dudumizi Technologies, tumekuwa tukipokea wateja wengi ambao wamekuwa wakilizwa au kukatishwa tamaa na hawa watu wa tekinolojia. Hivyo ili kuwasaia wengine, katika makala hii, tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapochagua mtoa huduma wa tekinolojia (IT).

1. Kadri uwezavyo, fanya shughuli na kampuni, na siyo mtu binafsi

Moja ya kitu cha msingi wakati unachagua mtoa huduma wa IT ni kuhakikisha unafanya kazi na kampuni na si mtu binafsi. Ingawa watu wengi wanaona kufanya kazi na mtu binafsi ni rahisi, lakini wengi wa watu binafsi hawa si wale walio makini na kazi yao, hivyo rahisi itakugharimu mno mno.
 Kwa mazingira na tabia za Watanzania wengi (siyo wote), huwa hatuna tabia ya kuangalia keshokutwa, kwani hata makampuni yenyewe mengi yanashindwa kuendeleza mahusianao na mteja, hivyo ni ngumu sana kuendeleza uhusiano wa kibaishara kati ya mtu na mtu.
Kwa kufanya kazi na mtu binafsi, inamaanisha, pindi mtu huyo atakapoumwa, kafariki au kupatwa na tatizo lolote basi huduma yako ndiyo imesimama.
Siyo tu kwa matatizo, tumekuwa tukipokea wateja wengi wengi kama Mabadiliko ForumsEBMC Game 1st Quality nk ambao imewabidi hata waamue kuachana na majina ya 
website zao kutokana na kutompata muhusika aliyewanunulia majina hayo au muhusika huyo kutopokea simu nk.

Tunaposema Kampuni, tunamaanisha si kampuni ya mfukoni, ni ile yenye ofisi, wafanyakazi na inafanya kazi kikampuni.
MUHIMU: Ingawa kufanya kazi na kampuni ni bora kuliko mtu binafsi, si kampuni zote ni bora na wala siyo watu binafsi wote ni longolongo, siku za usoni, tutaangalia mazingatio pindi unapochagua kufanya kazi na mtu binafsi (Freelancer)

2. Unapochagua kampuni, chagua kampuni iliyo bora


Kwakuwa tumeshaangalia faida za kuchagua kampuni badala ya mtu binafsi, hivyo, unapochagua kampuni, chagua iliyo bora. Chukulia mfano unataka kutengenezewa website, Kitu cha kwanza ni kutembelea website yao kuangalia wateja au kazi zao,baada ya kuridhishwa nazo, wasiliana na angalau mteja wao mmoja na upate maoni yake juu ya huduma zao, haswa huduma baada ya huduma (after sale service), nenda google na uandike jina la kampuni hiyo (google ni mtetezi wa wanyonge) na utaweza kuona nini kinaendelea kwao. Google haitoficha uovu wala uzuri wa kampuni.

Tembelea kurasa yao ya FacebookLinkedIn, Twitter nk uangalie muenendo wao. Wapigie simu kama mteja upate kujua uwezo na tabia zao kwa wateja. Na mwisho,jaribu kutembelea ofisi zao kujiridhisha na utendaji wao.

3. Hakikisha unapewa mkataba wa huduma
Ingawa wengi wetu tumekuwa tukilichukulia kama ni kitu cha kawaida, lakini mara nyingi limetuathiri sana, huduma za IT ni huduma ambazo ubora wake unanyumbulika sana, huduma hiyohiyo inaweza kutolewa katika viwango hata kumi na zote zikafanya kazi vyema katika ubora tofauti, hivyo, unapopewa huduma, hakikisha mumekubaliana juu ya kiwango cha huduma (SLA).
Kwa mfano, unapotengenezewa website, mtoa huduma lazima ahakikishe Website haina makosa (bugs) na ni salama, pia lazima ahakikishe inakuwa rafiki wa mitandao ya utafutaji (Search Engine Friendly) nk na kama siyo nini kinaendelea? Nani ataihudumia Website ikishamalizika? Nani atahusika pindininataka kuongeza kitu kwenye website...
Kama utafuatisha hatua hizi, basi utaweza kupata huduma iliyobora na itakayokuwezesha kufikia viwango vya ubora kwa biashara yako.
 Kwa makala zaidi za IT, Like kurasa yetu ya Facebook https://www.facebook.com/dudumizi

No comments:

Post a Comment