Sunday, July 13, 2014

WAZIRI MKUU WA TANZANIA, MHE. PETER MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

 Maafisa wa Ubalozi, Bwana Amos Msanjila na Dada Caroline Chipeta, Wakimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Pinda na Mkewe (Mama Tunu Pinda) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Peter Pinda akipokewa, kukaribishwa na kusalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Uingereza.

 Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano wao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda, alikutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai 2014, mara baada ya ziara yake fupi ya kikazi nchini humo.

Mkutano huo na Watanzania ambao uliofanyika Ubalozini, Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa taarifa mbalimbali za maendeleo nchini, hususan mchakato wa Katiba mpya, sera ya Diaspora na maandalizi ya chaguzi mbalimbali zinazokuja. Mkutano huo ulimalizika kwa maswali na majibu na baadae wananchi kupiga picha na Waziri Mkuu kama inavyoonekana kwenye picha hizi hapo chini.
 Watanzania waliofika kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda katika mkutano huo.
 Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania, wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, alipokutana na kuzungumza nao

Waziri Mkuu akijiandikisha kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi za Ubalozi

Mama Tunu Pinda, Mke wa Mhe. Waziri Mkuu akijiandikisha kwenye Kitabu cha Wageni Ofisini hapo.
 Pichani, Kaimu Balozi, Dada Caroline Chipeta (Mkuu wa Utawala), akiongea machache kumkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu

 Mtanzania, Bwana Chris Lukosi, akichangia na kutoa maoni yake kwa Watanzania wenzie waishio Uingereza
 Mke wa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akiongea na Watanzania waliofika kwenye mkutano wao na Mhe. Waziri Mkuu.
 Mhe. Waziri Mkuu na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi
 Maafisa wa Ubalozi, Wawakilishi wa Jumhuiya za Watanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Peter Pinda na Mkewe Mama Tunu Pinda


1 comment:

  1. Haya bwana waziri aje pia kututembelea wakazi wa kijiji cha mkanyageni

    ReplyDelete