Monday, July 28, 2014

UCHAGUZI DMV: SERA ZA MGOMBEA MAKAMU WA RAIS BI SALIMA MOSHI

Bi Salima Moshi

UZOEFU
Nina uzoefu wa kutosha katika maswala ya uongozi na maswala ya mawasiliano nimekuwa kiongozi wa muda mrefu katika upande wa sanaa na eneo langu ambalo nilikuwa naishi. Nimeweza kukuza na kuinua vipaji na wasaniimbalimbali ambao ni maarufu aidha kwa kudhihirisha kuwa ni kiongozi mtendaji na kuonyesha mfano niliweza kushiriki katika sanaa ya nyoka na kuliletea Taifa letu sifa pia vijana kupata ajira na kipato 
Mimi pia ni mzoefu katika mawasiliano kwa rika zote wakubwa wadogo vijana wazee wageni viongozi wa serikali kwa heshima na adabu kwa kuwaunganisha wote na kuleta umoja katika Jamii yetu.
              Nikiwa hapa DMV mimi na familia yangu tumekuwa tukisaidia wanajumuia kupata ajira na tumeshasaidia zaidi ya wanaJumuia zaidi ya 25 ili kuweza kujikimu na kuhamasisha kudumisha umoja katika jamii yetu.
 UMOJA 
Nitaimarisha network ndani ya Jumuia yetu ili kuwa kuwa pamoja na kuvunja makundi na kuwa karibu na Jumuia zote zilizopo DMV na STATE nyingine na kote DUNIANI 
 ELIMU 
Nitaishawishi serikali kupanua Uwigo wa kutoa mikopo ya Elimu ya juu hata kwa walio nje ili wana DMV waweze kufaidika na mikopo hiyo ya Elimu ya juu 
 DARASA LA KISWAHILI 
 Nitahakikisha tumepanga mipango madhubuti kuhusu darasa la kiswahili hasa kuhusu eneo la Darasa na Walimu na kuliendeleza hadi kwa vijana na kuwezesha kufungua darasa hata kwa watu wa hapa wanaotaka kujifunza kiswahili kwa kulipia ili jumuia kujipatia kipato Pia tutawafundisha watoto wetu wajue mila na Desturi zetu kwa kutumia taaluma yangu ya sanaaNitaanzisha kikundi cha sanaa kwa watoto na vijana ili waweze kujua Utamaduni wetu wa kucheza ngoma sarakasi maigizo nk Hapa DMV tuna vijana wanaweza kuimba kwaya na muziki wa Dansi tutaviendeleza vipaji vyao 
 AFYA 
 Nitasimamia upatikanaji wa BIMA Nafuu ya Afya kwa wana Jumuia kuwasiliana na mashirika mbalimbali ya Afya iliu wana Jumuia kuwe na utaratibu wa kuchekiwaAfya zao kila mwaka na kusaidiaWanajumuia kuwaelekeza maeneo kwa ajili ya huduma nafuu au ya bila malipo 
 AJIRA 
 Nitahakikisha nimesimamia Jumuia yetu kuwa na miradi Ambayo ya kuingizia kipato pia itasaidia wana Jumuia kupata ajira kama 7-11 kwa wenzetu MAKAZI Nitahakikisha Nimesimamia Jumuia kuweza kununua Nyumba kama mradi na wakati huohuo wanaJumuia kupata sehemu ya kuishi na kulipia katika Jumuia 
 DMV COMMUNITY CENTER 
 Nitahakikisha tumefungua community center yetu ili iwe sehemu ya kubadilishana mawazona kupata vyakula vya Nyumbani 
 MWANASHERIA 
 Nitasimamia upatikanaji wa mwanasheria wa Jumuia ili awe tayari kusaidia wana Jumuia katika maswala ya sheria 
 WAZEE Jumuia inahitaji Busara za wazee Nitahakikisha tumewashirikisha wazeena kukutana nao mara 2 kwa mwaka na kwa Enzi pia 
 ARDHI nitaishawishi Serikali kupitia wizara yake ya Ardhi kutupatia Eneo la Aridhi na kujenga kwa pamoja Nyumba za makazi kwa gharama nafuu kinakuwa kijiji cha wana DMV hiyo imewezekana kuna kijiji cha Wasanii Mkuranga
 MIKOPO 
 Nitazungumza na Bank mbalimbali Nyumbani ili wanaJumuia waweze kukopeshwa mikopo ya Nyumba au Biashara kwa marejesho nafuu 
 MAZISHI 
 Nitaishawishi serikali kuweza kuchangia gharama za Mazishi pale mwanaJumuia anapofariki kwa kutoa ubani wake kwani mwanaJUmuia anachangia kiasi kikubwa maendeleo nyumbani pia nitaongea na NSSF kuweza kukubali kupokea michango nusu nusu kwa dhamana ya JUMUIA na kupunguza kiasi kwa kuwa italipwa kama kikundi 
 URAIA PACHA 
Nitasimamia na kushawishi Serikali kupitisha uraia Pacha ili mTanzania aweze kuwekeza nyumbani bilakuonekana kama mgenindani ya NCHI yake Nitashirikiana na viongozi wote watakaochaguliwa ili tuweze kuleta maendeleo katika Jumuia yetu Ndugu wanaJumuia wenzangu mtakumbuka tulikuwa na kikao kwa Mhe. Balozi July 18, 2014  na kuhudhuriwa na board Tume na Wagombea Mgombea mwenzangu alitamka anajitoa na hataki kugombea tena huyu ni Nahodha kweli anabahatisha wakati wowote anaweza kuacha hataweza kuwavusha mifano tumeiona hatufanyi makosa tena mimi nitakua pamoja muda wote kwa hali yote kwa heshima naomba kura zenu ahasanteni

No comments:

Post a Comment