Tuesday, July 1, 2014

MTOTO WA MIAKA 9 ATAKA KUWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA NJIA NGUMU

Mzazi wa mtoto Idda Baitwa,Bw Respcius Baitwa akifanya maandalizi na mwanae ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya
kupanda Mlima Kilimanjaro
Mtoto Idda Baitwa akiwa na baba yake mzazi Bw Respcius Baitwa pamoja na ndugu zake wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya
kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mtoto Idda Baitwa akijiandikisha katika lango la Umbwe la kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.nyuma yake ni Bw Respicius Baitwa akshuhudia.
Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtoto Idda Baitwa ikaanza.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MTOTO wa miaka tisa(9) Idda Baitwa ameanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi huku akitumia njia ya Umbwe ambayo inaaminika kuwa ngumu zaidi kwa watalii wakati wa kupanda mlima huo.


Msichana huyo mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi Mnazi iliyoko Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro alianza safari hiyo Juni 28, mwaka huu ambapo ikiwa atafanikiwa kufika katika cha mlima huo atakuwa amaeweka rekodi mpya.


Akizungumza na Globu ya jamii wakati akianza safari ya kupanda mlima huo, katika lango la kupandia la Umbwe-Kibosho, Idda alisema matarajio ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mtanzania wa kwanza kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro katika umri mdogo kwa kupitia njia ngumu huenda sasa yakatimia.


Idda, alisema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuupanda mlima huo kama njia ya kuthibitisha uzalendo wake ambapo pia anaamini kwa kufanya hivyo atakuwa ametoa hamasa kwa watanzania wengine hususani wanawake kutembelea vivutio vya ndani.


Alisema ameamua kufuata nyayo za Baba yake ambaye tayari kwa sasa anajiandaa kuweka rekodi ya kuwa mtanzania na mwafrika wa kwanza kupanda vilele saba virefu katika mabara yalioko duniani ambayo hadi sasa ameshapanda vilele vinne.


"Nimekuwa nawaza juu ya azma yangu ya kuwa wa kwanza, nimekuwa nikimuona Baba akipanda milima nikawa natamani sana kufanya hivyo, nimechagua Njia hii ngumu kuliko zote kwa sababu nataka kuwaonesha watanzania wenzangu kwamba tunaweza na sio kuwaachia wageni pekee," alisema Idda.


Akizungumzia hatua ya Binti yake huyo  Baba mzazi wa Idda ,Respicious Baitwa aliishauri serikali kupitia wizara ya elimu kuweka msisitizo kwa wanafunzi mashuleni na vyuoni kutembelea hifadhi za taifa ili kujionea vivuito mbalimbali sanjari na kuwajengea hali ya uzalendo wa kupenda vitu vya
nyumbani.


Alisema ipo haja kwa serikali kupitia wizara ya elimu kuelekeza nguvu kwenye shule za msingii na vyuo kuwahamasisha wanafunzi kupanda mlima kilimanjaro kwa lengo la kuongeza hamasa ya watanzania kujitokeza kufanya utalii wa ndani.


"Sekta ya Utalii ina kazi kubwa sana ya kufanya, sio sekta hii tu hata Wizara ya elimu nadhani ni muda mwafaka sasa inatakiwa kujipanga na kuanza kuhamasisha wanafunzi mashuleni kupenda kutembelea vivutio vyetu, ipo haja ya kuongeza katika mnasomo mashuleni somo la utalii wa ndani na sio kuzungumza tu kwebnye vyombo vya habari," alisema Baitwa.


Kwa upande wake, LightnessSebastian, ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Mmbee iliyopo wilaya ya Mwanga, ameiomba wizara ya elimu kuongeza somo la utalii wa ndani katika mitaala ya elimu kwa lengo la kuwapa wanafunzi uelewaa wa utalii wa ndani

No comments:

Post a Comment