Tuesday, July 8, 2014

MAHAFALI YA SHULE YA AWALI YA OJAYS KIDDIES ZONE YAFANA

DSC_0401
Watoto wa shule ya Ojays Kiddies Zone iliyopo maeneo ya Kinondoni Block 41, wakiwa kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kuanza kwa mahafali ya Kaka na Dada zao wa Laura Class kuanzia miaka 4-5 (T-shrits za kijani) yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Regency Park jijini Dar mwishoni mwa juma.
DSC_0406
We are happy to Graduate....! Wanafunzi wa Laura Class wakipata Ukodak.
DSC_0640
Mkurugenzi wa Shule yaawali ya Ojays Kiddies Zone iliyopo Kinondoni -Block 41, Bi. Debbie Ndulla akiwakaribisha walezi/wazazi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0434
Baadhi ya walimu wa madarasa wakitambulishwa kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
DSC_0484
Walimu na wanafunzi wa Ojay Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi/walezi na waalikwa kwenye sherehe za mahafali hayo.
DSC_0723
Wazazi/walezi wakichukua Ukodak wa watoto wao kwenye mahaali hayo.
DSC_0494
Darasa la awali la Lilies Class wa miaka 1-2 wakitoa burudani ya kuimba kwa wazazi/walezi na wageni waalikwa kwenye mahafali ya kaka na dada zao.
DSC_0595
Mwenyekiti wa Bodi wa shule ya Ojays Kiddies Zone, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wazazi/walezi kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo ambapo aliwashukuru wazazi kwa kuonyesha kuwaamini na kuwapa fursa watoto wao kusoma kwenye shule hiyo yenye maadali bora na kuzingatia ustawi wa mtoto pindi awapo katika mazingira ya shule.
DSC_0623
Mwanaharakati wa Haki za Watoto, Zubeida Masabo akitoa nasaha kwa wazazi/walezi juu ya kuwalinda na haki za msingi ambapo aliwaasa kutenga muda wa kufuatilia maendeleo ya mtoto kila siku, amewashauri wazazi kuwa na taratibu za kutenga muda wa jioni kuzungumza na watoto wao kutokana kukithiri vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hali itakayosaidia kubaini vitendo vya uovu.
DSC_0619
Mmoja wa wazazi Dr. Isaac Maro akifafanua jambo kwa wazazi/walezi likiwemo suala la afya kwa watoto hasa magonjwa ambukizi kama Tetekuangua (chicken pox) ambapo wazazi wengi wamekuwa na hofu endapo kunatokea mlipuko wa ugonjwa huo kwenye mazingira ya shule wasihofu na kushauri watoto kuendelea kuhudhuria masomo kwani wakiumwa utotoni ni nafuu zaidi kutibika kuliko kuugua ukubwani.
DSC_0502
Watoto wa Lantana Class kuanzia miaka 3-4 wa shule ya awali ya Ojays Kiddies Zone wakijitambulisha mbele ya wazazi/walezi kwenye mahafali hayo.
DSC_0534
Kwa picha zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment