Wednesday, July 2, 2014

KAGASHEKI CUP 2014: WANABODABODA RWAMISHENYE FC WATEMA CHECHE TENA, WAIFUNGA TIMU YA NSHAMBYA BAO 4-0. KHALID SELEMAN AFUNGA HAT-TRICK!

Wachezaji timu zote mbili wakisalimiana Rwamishenye FC vs Nshambya FC

Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Rwamishenye Fc leo imeifunga Nshambya mabao 4-0 kwenye mchezo wao wa pili LIGI YA KAGASHEKI. Mtanange wao wa kwanza wa Ufunguzi wa Hii Ligi waliwanyuka bao 3-1 Mabingwa watetezi Bilele Fc 3-1.
Rwamishenye waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na makeke ya wachezaji wake ilijikuta Mchezaji wake Hatari Khalid Seleman akifunga bao zote Nne. 

Kipindi cha kwanza Khalid Seleman aliifungia bao mbili na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Nshambya. Kipindi cha pili tena akafunga bao mbili bao moja likiwa la penati.
Mapema leo mchana timu ya Bilele Fc Mabingwa watetezi aliifunga bao 1-0. 
Mashindano haya yataendelea tena kesho na kwa mechi mbili, Mechi ya kwanza itakuwa ni Hamugembe Fc vs Bakoba Fc saa 8:00 mchana na jioni sa 10:00 jioni ni Kahororo vs Kashai.
Waamuzi wa Mchezo huo Pamoja na Manahodha wa Timu zote mbili wakiteta kabla ya kuanza kipute jioni hii.
Waamuzi wa Mchezo huo Pamoja na Manahodha wa Timu zote mbili kwenye picha ya pamoja.Kikosi cha timu ya Bodaboda Rwamishenye.
Kikosi cha Timu yaNshambya Fc
Kocha Mkuu wa Timu ya Rwamishenye akiwapa somo wachezaji wake wa Rwamishenye FC Bw. Tegamaisho Deogratias, Hakuna kubweteka..na leo tunataka ushindi!!Kipute kilianza kwa kukamiana sana.
Mchezaji wa Rwamishenye Fc Seleman Khamis(kushoto) akichuana na Mchezaji wa Nshambya Odilo Gervase.Mashabiki waliingia kwa wingi Kaitaba leo
Siyo Kwamba Boda baoda zimeisha katika Kata ya Rwamishenye!! Hizi ni chache sana! ni za mashabiki kwani wamekuja kuwaangalia wenzao wanabodaboda wenzao wanasoka.

No comments:

Post a Comment