Thursday, June 19, 2014

WARSHA YA KUJENGA UWEZO WA MUZIKI NA SARAKASI KWA WATOTO NA VIJANA YATOLEWA


Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Center Bw.Mgunga Mwamnyenyelwa kilichopo mburahati kwa jongo wilaya ya kinondoni Dar es salaam, akizungumzia juu ya kituo hicho kinavyo fanya kazi na sababu za kuwakusanya watoto hao katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuwajengea uelewa zaidi na kuwafundisha vitu mbalimbali kama Ngoma, Sarakasi, ushonaji ili baadae waweze kuja kujitegemea wenyewe.

Meneja mradi wa Fit For Life Habiba Issa akielezea kwa kina juu ya Mradi huo pamoja na malengo yake

Daniela Titze International Relation Fit For Life
 Mani kutoka Ujerumani na ambaye pia ni Mwalimu wa Ngoma ya Brazil Samba Rege akielezea mafanikio na jinsi mafunzo yanavyo endelea.
Kikundi cha ngoma ndani ya kituo cha Baba watoto pamoja na wanafuzi waki achia burudani ya muziki aina ya Samba Rege
Mwalimu Daudi akiwa ana piga ngoma aina ya Samba Rege
Moja ya mambo yanayo fanywa katika kituo cha baba watoto utengenezaji wa maleba(costumes)
Vijana wakiwa katika mazoezi
Vijana wakifanya mafunzo ya serekasi katika kituo cha Baba watoto center

Kituo cha kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu cha Baba watoto center kupitia mradi wa FIT for –LIFE kinacho endesha mafunzo ya sanaa kwa watoto walio kati ya umri wamiaka 10 hadi 15 mpaka 25 aina ya mafunzo yanayo tolewa na pamoja na sarakasi ,muziki wa aina ya samba rage,kituo hicho kilichopo wilayani kinondoni  ambapo mradi huo ni wamiaka mitatu kutoka mwaka  2013 hadi mwaka  2016

Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyo andaliwa kwaajiri kuwafundisha vijana ambao nimaalumu kwaajili ya kuwa waalimu watakao weza kuwafundisha wanafunzi  katika kituo hicho mkurugenzi mtendaji wa kituo Ndugu Mgunga Mwamnyenyelwa ameeleza jinsi kituo hichokilivyo weza kuanzishwa katika maeneo ya mburahati  na wakazi wa maeneo hayo kuweza kufaidika na kituo hicho ,vilevile ameeleza changamoto wanazo kumbana nazo katika kituo hicho,

Mradi huo wa FFL unao fadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) ambao unaendeshwa  kwa hisani ya Goethe-Institute kama msimamizi mkuu amapo meneja wa mradi Habiba Issa ameeleza jinsi mradi huo unavyo endeshwa ikiwa lengo la mradi huu ni kuendeleza kukuza kwa vipaji kwa vijana na kuweza kujipatia fura mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa mwalimu katika sehemu tofauttofauti za mradi huo

Aidha meneja huyo bi. Habiba Issa amesema kuwa wameamua kuanzisha mrahi huu wa ili kuweza kuwasaidia vijana hususani walio maliza katika viwango mbalimbali vya elimu kwani wameweza kuwaandalia mazingira mazuri ya kujifunza uselemala,utengenezaji wa  maleba (costomes)kwaajili ya sanaa,uandaaji wa jukwaa(stage desgn) na matumizi ya mfumo wa sauti na mwanga katika maonyesho ya sanaa.

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Bw.Mgunga na Meneja Mradi wa FIT For the Fit Habiba Issa wameweza kutoa rai kwa wazazi na vijana mbalimbali waewez kutumia fursa zinazo onekana hata kufikia malengo yao waliweza kutoa mifano mbalimbali ambapo waliweza kuwataja wahitimu wallio hitimu na kuweza kuwa waalimu na wengine kutoka nne ya nchi ikiwa ni idadi ya zaidi ya wanafunzi 5 ambao waliweza kwenda nchini idia na nchi jirani,kwa wazazi wawe na moyo wa kuwaleta watoto ili waweze kupata elimu ya sanaa mbalimbali waache zana potofu ya kuwa sanaani uhuni usio kuwa na faida hayo yamesemwa na viongozi hao wa mradi huu.

No comments:

Post a Comment