Saturday, June 14, 2014

Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania watoa msaada kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili,Tandika jijini Dar

Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wameweza kujichangisha wenyewe kwa wenyewe na kupata fedha zilizofanikisha ukarabati wa jengo litakalotumika kama jiko la kupitia na ukumbi wa kulia chakula kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili cha Shule ya Msingi Tandika,Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,Wafanyakazi hao wameamua kufanya hivyo leo ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kusadia watu wenye Mahitaji,wanaofaunya mara moja kwa mwaka Duniani kote,mbali na ukarabati huo waliweza pia kujitolea kufanya usafi wa Mazingira ya eneo la Shule hiyo.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wakiwa wamejumuika pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandika ambao wanaulemavu wa Akili.
Wanafunzi hao wakifurahia ugeni huo uliowatembelea leo.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania wakifanya usafi wa Mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Tandika ambako kuna Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa Akili.
Usafi Ukiendelea.
Sehemu ya Ukumbi wa kulia Chakula kwa Watoto wenye Ulemavu wa Akili uliokarabatiwa na Wafanyakazi wa Citi Bank tawi la Tanzania ukiwa umepambwa tayari kwa kukabidhiwa Wenyewe
Baadhi ya Wafanyakazi wa Citi Banki wakiendelea kufyeka Majani katika eneo hilo.






Meneja Mkuu wa Citi Bank tawi la Tanzania,Noel Sangiwa (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa Akili Tandika,Mary Batamula (katikati) wakishirikiana kukata Utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo litakalotumika kama jiko la kupitia na ukumbi wa kulia chakula kwenye Kitengo cha Watoto wenye Ulemavu wa akili cha Shule ya Msingi Tandika,Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Watoto hao wenye Ulemavu wa Akili wakipelekwa kwenye Ukumbi wa Chakula.












No comments:

Post a Comment