Tuesday, May 20, 2014

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAUNGANA NA MKUU WA MKOA, NA MEYA WA KINONDONI KUFANYA USAFI MTO MLALAKUWA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) kukagua  mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wakati zoezi la kukagua mto wa Mlalakuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipata wasaa wa kupita na kumpa pole mkazi wa Mikocheni ambaye alikuwa amefiwa na Shemeji yake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda pamoja na wananchi walioungana nae, wakiangalia jinsi mto Mlalakuwa ulivyoharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiwahimiza kuhama wananchi wanaoishi pembezoni wa Mto Mlalakuwa kutokana na nyumba yao kubomoka na maji kama inavyoonekana.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakikagua mabanda ya mama lishe yaliyopo pembezoni mwa mto Mlalakuwa ambayo kwa kiasi kikubwa yapo katika hatarishi ya kuwapa wateja wao magonjwa yanayoambukiza.

  Hapa wakijionea jinsi maji machafu yanayotoka katika viwanda vilivyopo Mikocheni/Mwenge yakiingia katika Mto Mlalakuwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiongea na mmoja ya viongozi wa Kampuni ya Coca Cola jinsi ya kuwasaidia mama lishe wanaofanya biashara kuzunguka kiwanda hicho maana wapo katika mazingira magumu yanayoweza kuchangia mlipuko wa magonjwa wakati wakizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakielekea kuongea na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akitilia msisitizo suala la usafi kwa wakazi wa jiji ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakioungana na viongozi wao kufanya usafi ili kuweka jiji salama.
 Kila Mmoja akiwajibika.
 Zoezi la usafi halikujali rangi wala taifa...
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’  lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. 
 Mto Mlalakuwa ukiwa safi mara baada ya zoezi kumalizika.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. 
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) wakizoa uchafu na viongozi wa manispaa ya Kinondoni akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty (kulia) wakati wa zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty akiwa amebeba uchafu mara baada ya kumaliza kufanya usafi.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton pamoja na wananchi wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’  lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. 
Umati wa Wananchi waliohudhuria katika shughuli hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton akitoa shukrani zake za pekee kwa wananchi waliofika kufanya usafi pamoja.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio, Said Swale akiongea machache.
Mc Taji Liundi nae alipata nafasi ya kuongea macache.
Viongozi wa makampuni mbali mbali waliohudhuria wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’

No comments:

Post a Comment