Wednesday, May 21, 2014

TASWIRA MBALIMBALI UNAPOPANDA MLIMA KILIMANJARO KUPITIA NJIA YA LONDROS

Sehemu ya kwanza kabisa kuiona unapopanda mlima Kilimanjaro ni misitu uliotokana na kupandwa kwa miti inayotumika kwa ajili ya utengenezaji wa Mbao.
Baadae unaicha hiyo misitu kisha unakutana na uoto wa asili wa miti mifupi .
Kadri unavyo panda juu hali ya uoto inabadirika na hatimaye kukutana na nyasi fupi fupi iliyojishikiza kwenye miamba.
Kwa watali wa ndan sasa wanaweza tumia barabra maalum kupanda na magari yao kwenda kujionea mandhari ya mlima Kilimanjaro ukiwemo uoto huo wa asili na miamba.
Maua ya aina mbalimbali yanapendezesha maeneo hayo.
Hali ya hewa katika maeneo hayo hubadilika kila baada ya dakika kadhaa,wakati mwingine mnaweza msionane.
Wakati mwingine hali ni nzuri sana unatizama kila pembe ya mlima.
Mawe yaliyotokana na kurushwa kwa uji uliotokana na Volcano.
Maumbile mbalimbali ya vilima vilivyosalia kutokana na volcano hiyo.
Hali ya hewa inabadilika pole pole kila eneo utakalo pita.
Mabonde makubwa yaliyoambatana na mito kutoka katika miinuko ya mlima.
Viwanja vya ndege aina ya Helcopter katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uokoaji kwa watalii wanaopata matatizo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments:

Post a Comment