Thursday, May 1, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MKOANI RUKWA KATIKA UWANJA WA NELSON MANDELA MJINI SUMBAWANGA

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka (katikati) akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba kwa pamoja wimbo maarufu wa Wafanyakazi wa "Solidarity Forever"  na wafanyakazi walioshiriki maadhimisho hayo katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Rukwa wakiwaongoza wafanyakazi kuimba wimbo wa uishirikiano baina yao "Solidarity Forever" katika kuadhimisha Siku ya wafanyakazi duniani ambayo Kimkoa imefanyika mjini Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela.
Maandamano katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Wafanyakazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Chuo cha Ufundi Stadi VETA Katandala.
Idara ya Maji Sumbawanga (RUKWA) wakifanya vitu vyao.
NMB Sumbawanga.
SIDO Rukwa.
Chuo Kikuu Huria tawi la Rukwa.
Onyesho lililohusisha watoto wachanga mapacha katika kuonyesha utoaji huduma kwa mama wajawazito na watoto wachanga katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.
Onyesho la uharibifu wa mazingira kwa uchomaji misitu na ukataji miti ambalo hupelekea nchi kuwa jangwa na kuua vyanzo vya maji. Onyesho hili liliandaliwa na Idara ya Maji Rukwa.

Kikundi cha Ngoma za asili cha Kanondo kikiburudisha katika maadhimisho hayo.
Kikundi cha Waalimu kikiimba wimbo wa kutetea haki za wafanyakazi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

No comments:

Post a Comment