Sunday, May 18, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI YAENDELEA KUFANA KATIKA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UDAMADUNI JIJINI DAR

Kundi kubwa la wanafunzi kutoka shule mbali mbali wakisherekea Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani yanayo adhimishwa Kitaifa katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Kundi kubwa la Wanafunzi walio udhuria maadhimisho yaSiku ya Makumbusho Duniani katika Viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaama wakimsikiliza Mwendesha kipindi cha watoto, Bw Chance Ezekiel (Uncle Bilinge) hayupo Pichani.
Pichani ni Chance Ezekiel (Uncle Bilinge) na safu nzima ya uongozaji wageni wakiwa wanawanafunzi wa shule mbali mbali (hawapo pichani) katika kipindi cha Chemsha bongo na Burudani ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.
Mtaalam wa Makumbusho Anna Minja akitoa maelezo kuhusu Makumbusho kwa kundi la wanafunzi walio tembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni wakipokelewa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambapo kunafanyika maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Tanzania. 18 Mei.
Wataalamu wa Makumbusho ya Taifa wakiwa kwenye maandalizi ya Mwisho mwisho kabla ya Ufunguzi Rasmi wa Ukumbi wa Kudumu wa Sanaa uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Sehemu ya Ukumbi wa Kudumu wa Sanaa, unao tarajiwa kufunguliwa Rasmi hapo 18 Mei Makumusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment