Friday, May 16, 2014

KUNDI LA KWANZA LA WATALII WA NDANI MLIMA KILIMANJARO LAPANDA KILELE CHA SHIRA

Mabasi maalumu yanayotumika kupandisha watalii wa ndani yakiwa katika foleni tayari kwa safari ya kuelekea mlima Kilimanjaro katika kilele cha Shira.
Watalii wa ndani wakipatiwa maelezo juu ya mlima Kilimanjaro kablaya kuanza safari ya kuelekea Kilele cha Shira.
Watalii wa ndani wakiwa ndani ya basi kuelekea kilele cha Shira mlima Kilimanjaro.
Watalii wa ndani wakiwemo watalii wa kigeni wakijiandikisha katika kituo kilichopo Geti la Londros.
Moja ya basi likiwa na watalii wa ndani likipanda mlima Kilimanjaro kuelekea kilele cha Shira.
Wakiwa njiani watalii wa ndani walipata fursa ya kuchukua taswira katika mandhari mbalimbali ya mlima huo.
Mshindi wa ashindano ya urembo ya Miss Bikin Afrika Litha Cyprian alikuwa ni miongoni mwa watalii wa ndani waliopanda mlima Kilimanjaro.
Watalii wa ndani wakitizama mandhari ya mlima Kilimanjaro kwa mbaali wakitizama magari yakipandisha watalii.
Hatimaye safari kwa kutumia magari ikafika kikomo ili watalii wa ndani wakalazimika kutembea kwa miguu ili kufurahia hali ya hewa na madhari ya mlima,hapa wakipatiwa maelekezi ya mavazi ya kupandia mlima kutoka kwa muongoza watalii Alfred Kibiriti(mwenye miwani)
Safari ya kutembea mwendo wa dakika 45 kufika Shira hut ikaanza.
Hali ya hewa ilbadilika kila baada ya dakika 5.
Wengine walitafuta nguvu mpya kila walipoona mandhari ya mlima.hapa Mhifadhi Helen Mchack akiwangojea watalii wa ndani waliokuwa nyuma.
Hatimaye kundi la kwanza likafika katika kilele cha Shira.
Miongoni mwao alikuwemo Mshindi wa mashindano ya Urembo ya Miss Bikin Africa 2007.
Watalii wa ndani walipata nafasi ya kuingia katika mapango yaliyoko katika kilele hicho yajulikanayo kama Shira Caves.
Pata taswiras katika maeneo hayo.
Watalii wa ndani walijumuika na wataalii wa toka nje ya nchi kupata taswira katika eneo la Shira Camp.
Safari ya kurudi ikaanza baada ya kufurahia safari hiyo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazin.

No comments:

Post a Comment