Thursday, May 15, 2014

Kompyuta 230 zatolewa kwa ajili ya Skuli mbali mbali Unguja na Pemba

Kiongozi wa Wanafunzi 46 wa Skuli mbali mbali za Sekondari kutoka Nchini marekani waliopo Kiwengwa Zanzibar Bwana Criss Backam akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uwepo wao wa kujitolewa katika ujenzi wa skuli kupitia mradi wa Give Kutoka nchini humo.Kati kati yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna.
Jengo la Vyoo la skuli mpya ya Kiwengwa linayojengwa kupitia mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Marekani ambalo linajengwa kwa kutumia Taaluma ya Chupa za maji safi ya kunywa iliyobuniwa Nchini Nicaragua Amerika ya Kusini.
Jengo la skuli mpya inayojengwa katika Kijiji cha Kiwengwa ndani ya Jimbo la Kitope kupitia Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Nchini Marekani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwashukuru na kuwapongeza Wanafunzi wa skuli mbali mbali za Sekondari Nchini Marekani ambao wapo Zanzibar wakijitolea katika mradi wa ujenzi wa skuli mpya ya Kiwengwa.
Balozi Seif, Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamhuna wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa kujitolea kutoka skuli mbali mbali za Sekondari Nchini Marekani hapo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiembe Samaki walioshuhudia hafla ya Wizara ya Elimu kakabidhiwa Kompyuta 230 kwa ajili ya skuli mbali mbali za Zanzibar kutoka Rotary Klabu ya Kimataifa ya Mji wa Seattle Nchini Marekani.
Baadhi ya msaada wa Kompyuta zilizokabidhiwa Wizara ya Elimu kwa ajili ya Skuli za Zanzibar zikitoka Rotary Klabu ya Kimataifa ya Mji wa Seattle Nchini Marekani.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi akisherehesha kwenye hafla ya makabidhiano ya Kompyuta kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar hapo Makao Makuu ya Wizara ya Elimu Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna akitoa shukrani zake kwa taasisi hisani zilizojitolea kusaidia Kompyuta pamoja na vifaa vyake kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Ni baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Wazanzibari na Watanzania walioko Mjini Seattle Nchini Marekani ambavyo viliambatana na msaada wa Kompyuta zilizotolewa na Rotary Klabu ya Mji huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Waziri wa Elimu Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna Msaada wa Kompyuta 230 zilizotolewa msaada ya Rotary Klabu ya Seattle Nchini Marekani kufutia ziara yake aliyoifanya ya Mwezi Novemba mwaka jana.
Balozi Seif akimkabidhi Waziri Shamhuna Baadhi ya Vitabu vilivyotolewa na Wazanzibari na Watanzania walioko Mji wa Seattle Nchini Marekani ikiwa ni msaada kwa wanafunzi wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment