Sunday, May 18, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA MKOA WA TABORA KWA KUHUTUBIA MKUTANO MKUBWA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Tabora leo, ambapo aliwananisha wapinzani na Boko Haramu wa waasi wa Nigeria kwa kuwachonganisha wananchi kwa maneno kitendo ambacho alidai nkinaweza kusababisha vurugu nchini.
 Wananchi wa Kijiji cha Inala, Manispaa ya Tabora  wakimsikiliza Kinana akihoji sababu zilizosababisha ujenzi wa mfumo wa umwagiliaji kuchelewa kukamilika licha ya mkandarasi kulipwa sehemu kubwa ya malipo.
 Kinana akihudumiwa na Mama Lishe alipokwenda kula yeye na msafara wake kwa akina mama lishe eneo la Stendi Mpya Tabora mjini. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa wakipata mlo kwa Mama Lishe mjini Tabnora leo.
 Waandishi wa habari walio kwenye msafara wa Kinana, Said Mwishehe (kushoto) na Jingu wa Radio Uhuru, wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe leo mjini Tabora.
 Ni wakati wa msosi kwa mama lishe mjini Tabora
 Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Edward (kushoto) na dereva wa katibu huyo, Prosper 9wa pili0 kushoto0 wakiwa na wanahabari walio kwenye msafara wa Kinana, Anne Robi wa Daily News pamoja na Said Mwinyimkuu wa Clouds TV wakipata mlohu huo wa machana kwa Mama Lishe mjini Tabora. 
 Mbunge wa Jimbo la Tabora, Aden Rage (kushoto) akiungana na Kinana kula msosi kwa mamaLishe mjini Tabora leo.
 Kinana akinawa baada ya kupata msosi huo wa nguvu kwa Mama Lishe
 Kinana akiongoza msafara wake kwa miguu kutoka kwa akina Mama Lishe kwenda kwenye mkutano wa hadhara Stedi ya Zamani ya Tabora
 Kinana akiwasalimia wananchi alipkuwa akiwasili kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Waziri Ummy Mwalim akihutubia  katika mkutano wa hadhara na kuuponda Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka bungeni kwa sababu zisizoeleweka wakati wa Bunge la Katiba.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM, ambapo aliimpongeza Katibu Mkuu Kianana kwa kufanikisha ziara yake mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Tabora, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyama vya Ushirika nchini (WETCO), Wakasubi kwa hotuba yake nzuri Mwassa alisema wakulima wasibanwe kuuza tumbaku kwa mnunuzi wanayemtaka, Pia alitaka wakulima walipwe fedha zao zote wanazodai kwa vyama vya ushirika.
 Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akihutubia katika kutano huo na kusisitiza kwamba watu wote waliohusika kuwadhulumu wakulima fedha za tumbaku wakamatwe mara moja na kushitakiwa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwaponda viongozi wa Ukawa wa kususia mkutano wa Bunge la Katiba. blia kuwa na sababu za msingi.
 Baadhi ya wasanii wakishiriki kwenye mkutano huo
Kinana akimpongeza Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Tabora, Wakasubi alipokuwa akienda jukwani kuhutubia. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment