Thursday, May 22, 2014

BENKI YA CRDB YACHANGIA MILIONI 20 UJENZI WA KANISA LA KKKT JIMBO LA HAI

 Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa  akiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jimbo la Hai kwa ajili ya ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT jimbo la Hai. Katika harambee hiyo Benki ya CRDB ilitoa shilingi milioni 20 kufanikisha ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Baadhi ya waumini wakiingia kanisani wakati wa ibada maalumu ya iliyofanyika katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai, iliyokwenda sambasamba na harambee ya kuchangia kanisa hilo pamoja na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakiwa katika ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kanisa la KKKT jimbo la hai.
  Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na Askofu wa KKKT jimbo la Kaskazini, Dk. Martin Shao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoisha katika mazingira magunu
Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa  (kushoto), akimkabidhi  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei sehemu ya fedha zilizopatikana katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Kanisa la KKKT Jimbo la Hai. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki.Kulia ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao. 

No comments:

Post a Comment