Baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Shanghai nchini China wamesherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania kwa kukutana pamoja na kuzungumza mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Licha ya sherehe hizo za Miaka 50 ya Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kumaliza mwaka huu.
Baadhi ya Watanzania waishio Shanghai wakipiga picha ya pamoja katika shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanzania,yaliyofanyika jana.
Baadhi ya Watanzania wanaomaliza masomo yao mwaka huu wakipiga picha ya pamoja mbele ya keki ya Muungano.
Mmoja wa wahitimu Bi. Hellen Shayo akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Watanazania waishio Shanghai cha kuwa mwanachama hai kwa kipindi chote alichokuwa hapa.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria sherehe za Muungano.
Watanzania wakikata keki ya Muungano huku wakiwa wa nyuso za bashasha zinazodhihirisha umuhimu wa siku hiyo adhimu.
Wakipata chakula.
wakiyarudi magoma kusherehekea Muungano.
Mdau wako wa nguvu akifurahia siku hii adhimu.
Baadhi wageni waalikwa.
Hongereni sana kwa uzalendo huu!
ReplyDeleteSafi sana vijana. Uzalendo ni jambo zuri sana. Asanteni kwa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania. So proud of u guys....
ReplyDeleteMnastahili tuzo mrudipo nyumbani. Big up sana.
ReplyDeleteHongereni kwa kuwa wazalendo, Hongera viongozi na wote mliofanikisha.
ReplyDeleteThats great!
ReplyDeletemmepeperusha vyema Bendera ya Tanzania.mmekuwa mfano mwema.
Muungano Daima!
Uzalendo 100%
ReplyDeleteEneza upendo na ukarimu wa nchi yetu daima.
Proudly Tanzanian
Yani hawa vijana wamenipa raha ya ajabu. is there a way for these guys to be recognized na serikali once they come back? this is not the first time naona vijana wanaofanya masomo yao China wakiitangaza nchi yetu. inabidi serikali itambue mchango wao jamani. Kazi nzuri watz wenzetu. keep up the spirit.
ReplyDeleteMmenikosha sanaaaaaaaa
ReplyDelete