Thursday, April 3, 2014

MAAFISA TUME WAFUNZWA STADI ZA UCHUNGUZI

Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki akifungua rasmi mafunzo ya stadi za uchunguzi yanayofanyika katika hoteli ya Naura Spring jijini Arusha. Mafunzo hayo ya wiki moja kuanzia Machi 31—4, 2014 yamelenga kuwaongezea maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) stadi za kiuchunguzi hasa wanapofanya uchunguzi unaohusiana na kazi za kila siku za Polisi. kushoto ni muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi. Lindiwe Khumalo na kulia ni Muwezeshaji Mkuu wa mafunzo hayo Bwana Sean Tait kutoka African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF).Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la GIZ.
Sehemu ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto ni Afisa Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Sheria, Bwana Nabor Assey na anayeonekana kwa mbali ni Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula.
Maafisa wa THBUB wakimsikiliza kwa makini Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait (hayupo pichani).Kutoka kushoto ni Bibi Monica Marealle (katikati) ni Bwana Elias Sowani na (kulia) ni Bwana Pontian Kitorobombo.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiongea na Maafisa wa THBUB wanaoshiriki mafunzo(hawapo pichani) na kuwataka kuwa wasikivu ili kwa pamoja waweze kupata faida kutokana na mafunzo hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki.
Maafisa Uchunguzi wa THBUB wakijifunza kwa vitendo namna ya kukabiliana na Matukio yanayohusiana na uvunjwaji wa haki za binadamu.
Muwezeshaji wa Mafunzo kutoka THBUB, Bibi Jamila Sulu akiwapa maswali ya “chemsha bongo” Maafisa wa THBUB kwa lengo la kupima kumbukumbu ya kile walichojifunza.
Muwezeshaji kutoka African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF) akiwasilisha mada inayohusu Uandaaji wa ushahidi Mahakamani.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiwasilisha Mada ya kwanza inayohusu Haki za binadamu na masuala ya Polisi.
Maafisa wa THBUB wakijadiliana katika kazi za vikundi ambazo ni sehemu ya Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala Bora, Hajat Fatuma Muya akichangia jambo katika mafunzo hayo.Anayemsikiliza ni Afisa Uchunguzi, Bi. Farida Ndege.
Maafisa Uchunguzi wa THBUB wakifanya mafunzo kwa vitendo kutoka ( Kushoto) ni Bi. Vivian Method na (kulia) ni Bi. Makihiyo Mrutu.
Sehemu ya washiriki wakipitia makabrasha wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi Lindiwe Khumalo akichangia jambo katika mafunzo hayo, kulia ni Muwezeshaji Bi. Louise Edwards.
Maafisa Uchunguzi wa THBUB katika kazi za vikundi wakati wa mafunzo.
Bwana Mokgapi Maleka , Afisa kutoka shirika la GIZ la Afrika Kusini ambalo ndio wafadhili wakuu wa Mafunzo hayo akiongea na washiriki.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji.

No comments:

Post a Comment