Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza mamia ya waombolezaji na viongozi mbalimbali wa Serikali na JWTZ katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna wa Jeshi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Marehemu Meja Jenerali Kelvin Msemwa iliyofanyika uwanja wa makao makuu ya Jeshi, Upanga, Dar es salaam, April 6, 2014. Marehemu alifariki dunia April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. Mwili wake unasafirishwa kuelekea Songea kwa mazishi April 7, 2014
Majenerali Wastaafu na walio kazini
Majenerali wastaafu na walio kazini
Jukwaa kuu
Rais Kikwete akiwa jukwaa kuu na viongozi wengine mbalimbali
Mama Salma Kikwete akiwa jukwaa kuu
Sehemu ya jukwaa kuu
Viongozi waliopata kuwa Mawaziri wa Ulinzi Profesa Philemon Sarungi na Dkt Emmanuel Nchimbi na viongozi wengie
Viongozi wa sasa na waliostaafu
Waombolezaji
Kikosi kazi cha maandalizi na utekelezaji
Mwili ukiwasili
Gari la mzinga likiwa limebeba mwili wa marehemu
Maafisa waandamizi wasindikizaji wa mwili wa marehemu
Mwili ukitelemshwa kutoka katika gari la mzinga
Hema kuu inasimama kama ishara ya heshima kwa marehemu
Jemedari Mkuu na viongozi wengine
Amiri Jeshi Mkuu akielekea kutoa heshima zake za mwisho
Amiri Jeshi Mkuu Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho
Wakitoa pole kwa wafiwa
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akielekea kutoa heshima zake za mwisho
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akitoa heshima zake za mwisho
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akimfariji mjane wa marehemu
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akielekea kutoa heshima zake za mwisho
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akitoa heshima zake za mwisho
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akimpa pole mjane wea marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akielekea kutoa heshima zake za mwisho
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima zake za mwisho
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimpa pole mjane wa marehemu
Wakuu wa mikoa ya Dar es salaam (kulia Mhe Saidi Mecky Sadid) na Mtwara (Kanali Joseph Simbakalila) wakitoa heshima zao za mwisho
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima akitoa heshima zake za mwisho
Heshima za mwisho
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Albert Ndomba akitoa heshima zake za mwisho
Profesa Philemon Sarungi na Dkt Emmanuel Nchimbi wakitoa heshima zao za mwisho
Wafiwa wakipewa mikono ya pole
Mikono ya pole kwa wafiwa
Wanadhimu Wakuu Wastaafu wa JWTZ Luteni Jenerali Sayore na Luteni Jenerali Iddi Gahhu wakitoa heshima zao
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert Mboma akitoa heshima
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert Mboma akitoa pole kwa mjane wa marehemu
Heshima ya mwisho kwa marehemu
Saluti ya mwisho kwa marehemu
Majenerali walio kazini na wastaafu wakielekea kutoa heshima zao za mwisho
Heshima za mwisho kwa marehemu
Pole kwa wafiwa
Maafisa waandamizi wakimuaga mwenzao
Wakitoa pole kwa wafiwa
Poleni sana....
Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu
Maafisa waandamizi wakielekea kutoa heshima
Kuelekea kutoa heshima za mwisho
Waambata wa kijeshi katika balozi mbalimbali walikuwepo
Heshima za mwisho toka kwa waambata wa kijeshi
Mjane wa marehemu akipelekwa kuaga mwili wa marehemu
Jeneza likifungwa baada ya heshima za mwisho
Mwili ukiandaliwa baada ya heshima za mwisho kutolewa
Mwili ukiondolewa baada ya heshima za mwisho
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio
Amiri Jeshi Mkuu akisindikizwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiagwa na maafisa waandamizi wa JWTZ
Poleni wakuu kwa kuondokewa na kipenzi chenu
ReplyDelete