Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati katika mto Mtokozi . Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa hapa jijini.
Hapo jana siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.
Siku ya Jumatatu daraja jingine katika katika mto Kizinga kwenye barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Kongowe ilifunguka baada ya kazi ya usiku kucha iliyoongwozwa na Waziri Magufuli kufanikisha kukamilisha matengenezo katika sehemu hiyo yenye magari mengi. Barabara ya Kilwa ndiyo kiungo kikuu cha usafiri wa barabara kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.
Aidha katika siku hiyo hiyo ya Jumatatu, daraja la Ruvu pia lilianza kupitisha bagari baada ya sehemu ya barabara iliyokuwa imeharibika kutokana na mafuriko, kukarabatiwa.
Matengenezo yakiendelea katika Daraja la Mpiji.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matengenezo katika Daraja la Mpiji.
Waziri Magufuli akijionea madhara ya mafuriko katika barabara ya Kilwa eneo la mto Mzinga eneo la Mbagala Kongowe.
Waziri Magufuli akiwa kazini usiku katika eneo la mto Kizinga.
Hali ilivyo sasa katika eneo la Mto Kizinga kwa sasa.
Hali ilivyokuwa katika daraja la Mto Mtokozi katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.
Hali ilivyo sasa katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.
magufuli jembe mm ni mzanzibar kama anapewa aongoze znz magufuli mwaka mmoja nchi itanyooka ile hali ya znz siku inaanza saa 4 na kazi kwisha saa 9 na nusu itaondoka tunahitaji znz tuwe na magufuli wa 3 znz nchi ipate maendeleo sio siasa uchumi haukui kwa siasa chafu
ReplyDelete